Kuunganishiwa Umeme Sasa Kuanzia Sh180,000
Posted in
No comments
Saturday, July 28, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
PROF. SOSPETER MUHONGO-WAZIRI WA NISHATI NA MADINI |
SERIKALI
imetangaza kushusha gharama za kuunganisha umeme kwa wananchi
wanaohitaji huduma hiyo kwa viwango ambavyo ni kati ya asilimia 60 na 77
kwa wakazi wa vijijini na kati ya asilimia 29 na 65 kwa wananchi
waishio sehemu za mijini.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliliambia Bunge jana
kuwa gharama za kuunganishiwa umeme kwa wateja walioko kwenye umbali
usiozidi meta 30 (single phase) ambao hawahitaji nguzo sasa zitakuwa
Sh177,000 kwa wateja wa vijijini na mijini itakuwa Sh320,960 badala ya
Sh455,108 ambazo zilikuwa zikilipwa awali bila kujali mteja aliko.
Akiwasilisha
hotuba ya makadirio ya matumizi ya wizara yake ya 2012/2013 bungeni
Dodoma jana, waziri huyo alisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 61.11
kwa wateja waishio vijijini na asilimia 29.48 kwa wateja waishio mijini.
Profesa
Muhongo alisema pia Serikali imeshusha gharama za uunganishaji wa umeme
kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) na kuwekewa nguzo
moja katika maeneo ya vijijini ambao sasa watalipa Sh337,740 na mijini
Sh515,618 badala ya Sh1,351,884 zilizokuwa zikilipwa awali.
“Punguzo
hilo la pili ni sawa na asilimia 75.02 kwa wateja wa vijijini na
asilimia 61.86 kwa wateja waishio mijini,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema
kwa wateja watakaojengewa njia moja na kuwekewa nguzo mbili katika
maeneo ya vijijini watalipa Sh454,654 na mijini watalipa Sh696,670
badala ya Sh2.001 milioni zilizokuwa zikilipwa awali.
“Punguzo
hili ni sawa na asilimia 77.28 kwa wateja waishio vijijini na asilimia
65.19 kwa wateja waishio mijini,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza.
“Viwango hivyo vya gharama vitaanza kutumika Januari mwakani bila
kisingizio.”
Chimbuko la Punguzo
Hatua
ya kushushwa kwa gharama za kuunganishiwa umeme zimekuja zaidi ya mwaka
mmoja tangu Rais Jakaya Kikwete alipolilekeza Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco), kupunguza gharama hizo ili kupata wateja wengi zaidi.
Machi
18 mwaka jana, Rais Kikwete aliitaka Tanesco, kupunguza gharama za
kuunganisha umeme kwa wananchi ili wengi wapate huduma hiyo sambamba na
kuongeza wateja wanaotumia umeme kwa asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
Akizungumza
na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini, Rais Kikwete alisema
gharama hiyo ikipunguza, itaiwezesha Tanesco kupata wateja wengi
ikilinganishwa na sasa.
Kauli
ya Rais ilitokana na maelezo ya Mkurugenzi wa Shirika hilo, William
Mhando (ambaye sasa amesimamishwa kazi) kuwa Tanesco ilikuwa ikifanya
mazungumzo na Benki za Akiba na Azania ili zitoe mikopo kwa wateja kwa
ajili ya kuunganishiwa umeme.
Chanzo. http://www.mwananchi.co.tz
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :