MABASI MAKUBWA YAGOMEA USHURU MPYA ULIOTANGAZWA NA MANISPAA YA MOSHI
Posted in
No comments
Sunday, July 1, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
IKIWA ni takribani wiki mbili tu tangu mji wa moshi
ulipokumbwa na adha ya usafiri baada ya madereva wa daladala kufanya mgomo, mji
huo umejikuta ukionja machungu hayo kwa mara nyingine tena safari hii, ikihusisha
mabasi makubwa.
Madereva hao kama ilivyokuwa kwa wenzao wa daladala,
wamegoma kuheshimu ombi la kulipa ushuru wa Tsh. 2000 kama ilivyoainishwa
katika tangazo la manispaa ya moshi ya tarehe 18 juni mwaka huu ikiwataka
kulipa ushru wa maegesho ya Tsh. 2000 toka katika ile ya ada ya kawaida ya Tsh.
1500.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya madereva hao walisema
kuwa kilichowapelekea kugomea ushuru huo ni kitendo cha manispaa kupitisha
maamuzi yake bila ya kuwashirikisha.
Walisema wao kama wadau wakubwa hawajapokea taarifa zozote
za kimaandishi kutoka kwa manispaa kuwajulisha kuhusa uwepo wa mabadiliko ya
tozo hiyo na kwam,ba cha kinachowafanya wawe na maswali mengi ya kuhoji ni
kitendo cha wamiliki wao kutowapa maelezo yoyote kuhusu mabadiliko hayo ya
ghafla.
“Hapa sisi kwa kweli hatuelewi hii serikali inaendeshwaje,
maana haingii akilini kwa chombo kama manispaa kufanya maamuzi bila
kutushirikisha wadau katika maamuzi yao, sasa weaop wanadhani hiyo hele na
uchumi huu itatoka wapi,’” alihoji moja wa madereva hao ambaye hata hivyo
hakutaka kutaja jina lake.
Katibu wa TABOA,
Ainea Mrutu alipoulizwa kuzungumzia mgomo huo, alisema yeye binafsi hakubaliani
kile kitendo cha kupandishwa kwa ushuru na kuongeza kuwa kinachoendelea katika
kituo hicho haiendani na hali halisi ya uchumi katika kituo hicho.
Alisema anashangaa ni kwa nini manispaa inan’gan’gania kupandisha
ushuru wakati suala hilo limeshaongelewa kwa pamoja na wadau wote chini ya mkuu
wa wilaya na kuitaka manispaa kuangalia swala hilo kwa umakini ili kuepuka mgogoro
usiokuwa wa lazima.
“Unajua swala hili linanishangaza sanma halafu sijui ni kwea
nini manispaa bado inaendelea kutoza ushuru huu wakati katika kikao cha tarehe
25 tulishakubaliana kumwomba mkuu wa wilaya kukutana na barua nimeshaandika
kinachosubiriwa ni majibu yamkuu wa wilaya, nawashauri manispaa kusubiri
kwanza,” alisema Mrutu.
Kwa upande mwengine, mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa
wa Kilimanjaro, Christopher Lyimo, akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu,
alisema kuwa yeye kama yeye hayupo katika nafasi ya kulizungumzia kutokana na swala
hilo kwa sasa kuwa katika mikono ya mkuu wa wilaya ya moshi.
“Mimi kama mimi siwezi kulizungumzia na nadhanio hata
manispaa wangesubiri kwanza tukutane na mkuu wa wilaya kulijadili swala hili,”
alisema Lyimo.
Mgomo huo unakuja siku chache tu baada ya ile ya daladala
zinazofanya safari mjini hapo kupinga ongezeko la ushuru ambapo kwa mujibu
watangazo la manispaa kwa vyombo vya usafiri ilitangaza kupandisha ushuru ya
maegesho kwa magari yote yanayoingia na kutoka katika kituo hicho.
Kabla ya ongezeko hilo daladala zilikuwa zinalipa shilingi
1000, mabasi shilingi 1500 na magari madogo ya abiria, teksi yal;ilipa shilingi
kama ushuru ya maegesho lakini kwa sasa katika tangazo hilo lililoanza kufanya
kazio tarehe 01 julai mwaka huu, walitakiwa kulipa shilingi 1500 kwa daladala,
shilingi 2000 kwa magari makubwa na shilingi 500 kwa teksi.
Juhudi za kumpata mstahiki meya wa manispaa ya moshi,
mheshimiwa Jafari Michael, kulizungumzia swala hilo kutoka na mkurugezi wa
manispaa hiyo, Bernadeta Kinabo kuwa nje ya manispaa kwa sababu za kikazi
hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita bila kupokelewa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :