Mkuu wa Jeshi afutwa kazi
Posted in
No comments
Monday, July 16, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Mkuu wa majeshi wa Korea Kaskazini ameondelewa madarakani, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo.
Ri Yong-Ho alipewa wadhifa huo miaka miwili iliyopita, kabla ya kifo cha kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini Kim Jong-il.
Kuondolewa kwake mamlakani kunaangaliwa kama ishara ya mwelekeo wa utawala wa mwanawe kiongozi huyo wa zamani Kim Jong ill .
Shirika la Habari la serikali lilisema Bwana Ri amevuliwa madaraka yote ya kijeshi na kisiasa.
Mbali na kuwa mkuu wa Jeshi, naibu mwenyekiti wa
tume Kuu ya jijeshi, yeye pia alishikilia vyeo kadhaa vikuu katika
chama kinachotawala cha Workers Party.
Katika taarifa fupi chama hicho kilisema kiliamua kumwachisha madaraka yote Bwana Ri Yong kwa sababu ya ugonjwa.
Hata hivyo chama hicho hakikutoa taarifa zingine
lakini ni wachache wanaamini kuwa ametimuliwa vyeo hivyo vyote kwa
sababu ya maradhi pekee.
Bwana Ri alikabidhiwa madara ya Mkuu wa majeshi miaka mitatu iliyopita.
Alionekana mara nyingi karibu na kiongozi wa
zamani, Kim Jong Il, na alidhaniwa kuwa angalikuwa kiungo muhimu katika
kumkabidhi madaraka mwana wa kiongozi huyo, Kim Jong-un.
Kim-Jong-un, ambaye ametawala sasa kwa miezi sita, anaaminika kuwa na umri chini ya miaka 30.
Lakini Kim Jong-un anadhaniwa kuwa huenda
akaanzisha mabadiliko kwa sababu uongozi wake unaoonekana kuwa bila
ukakamavu wa baba yake.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :