Dlamini-Zuma ampiku Ping Addis Ababa
Posted in
No comments
Monday, July 16, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Nkosazana Dlamini-Zuma, kutoka Afrika Kusini, ameshinda uchaguzi mkali kuwa kiongozi mpya wa Tume ya Muungano wa Afrika.
Bi Nkosazana Dlamini-Zuma, alimshinda kiongozi
wa Tume hiyo anayeondoka Jean Ping wa Gabon, katika uchaguzi mkali
uliopigwa mara kadhaa.
"hivi
sasa tunaye kiongozi wa Tume ya Muungano wa Afrika Madam Zuma, ambaye
sasa ataongoza siku za usoni za taasisi hii," ndivyo alivyosema Rais wa
Benin Thomas Boni Yayi ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika
AU.
Dlamini-Zuma, mwenye umri wa miaka 63, ni balozi
mwenye ujuzi na alikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru nchini
Afrika Kusini wakati wa Ubaguzi wa rangi.
Yeye ni daktari wa mwanadamu na amewahi kuhudumu
kama Waziri wa Afya, Maswala ya Nchini na waziri wa Mashauri ya nchi za
Kigeni nchini Afrika Kusini.
Zuma ampongezab Dlamini
Mumewe wa zamani, ambaye pia ni kiongozi wa
Afrika Kusini, Jacob Nzuma, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza
kumpongeza kwa ushindi huo baada ya kura kupigwa katika mji mkuu wa
Ethiopia, Addis Ababa.
Rais Zuma alisema; "Ushindi huu ni ufanisi mkubwa kwa Afrika, bara zima, umoja na mafanikio kwa wanawake ni muhimu sana."
Ushindi wa Dlamini-Zuma umepatikana miezi sita tangu aanze juhudi za kumtimua mwenyekiti wa tume hiyo anayeondoka, Jean Ping.
Katika mkutano kama huo kura ilipopigwa hakuna mmoja kati yao aliyepata thuluthi mbili ya kura kumwezesha kunyakua uongozi huo.
Iliamuliwa kuwa Ping aendelee kushikilia cheo hicho hadi usiku wa kuamkia leo aliposhindwa na Dlamini-Zuma.
Rais Yoweri Museveni alishangilia kwa kusema: "huyu ni mpiganiaji Uhuru na si balozi wala kiongozi vivi hivi."
Msemaji wa Ping, Noureddine Mezni, alisema Bwana
Ping alimpongeza Madame Dlamini-Zuma na kumtakia kila la heri katika
kazi yake mpya.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :