Wazee wa Maumau wawasilisha kesi London
Posted in
No comments
Monday, July 16, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Kundi la wazee kutoka nchini
Kenya wanaodai kuwa walinyanyaswa na kuteswa na utawala wa kikoloni wa
Uingereza takriban miaka hamsini iliyopita wamewasilisha kesi yao mjini
London.
Mwaka mmoja uliopita Mahakama iliamuru kuwa
Serikali ya Uingereza haiwezi kujibu tuhuma za vitendo vya watumishi wa
Mamlaka ya ukoloni.
Wapiganaji hao ambao wanadai kunyanyaswa na serikali ya kikoloni wakati wakipigania uhuru wa Kenya kutoka kwa Uingereza.
Wazee hao walikuwa wapiganaji wa kundi la Maumau
ambalo lilishiriki harakati za uhuru wa Kenya zaidi ya miaka hamsini
iliyopita wanasema waliteswa.
Wanadai kuwa maafisa wa Kikoloni wa Uingereza
waliwatendea vitendo vya kinyama ikiwemo kuzuiliwa katika
kambi,kupigwa,kudhalilishwa kijinsia na hata baadhi ya wanaume kufinywa
sehemu zao za siri.
Yote hayo wanasema ni kwa sababu walipinga utawala wa kikoloni.
Yote hayo wanasema ni kwa sababu walipinga utawala wa kikoloni.
Sasa wanataka serikali ya Uingereza iwalipe
fidia kutokana na mateso hayo. Mawakili wanaowakilisha kundi hilo
wanasema wateja wao ni sehemu ndogo ya mamia ya washiriki walio hai kwa
sasa nchini Kenya ambao walipitia mateso kama hayo. Wenzao wengine
walifariki katika miaka iliyopita.
Awali serikali ya Uingereza ilikuwa imesema
haiwezi kuchukua lawama kwa vitendo vilivyotendwa na a utawala wa
kikoloni kati ya mwaka 1950 na 1960.
Hata hivyo mwaka jana Jaji wa mahakama kuu mjini
London akatoa uamuzi kuwa kesi ya wapiganaji hao wa zamani ina msingi
na inapaswa kusikilizwa.
Sasa wapiganaji hao watapata fursa ya kutoa
ushahidi wao mahakamani kupitia wenzao Ndiku Mutua, Paulo Nzili, Wambugu
wa Nyingi na mwanamke pekee Jane Mara wote ambao wamefika hapa London
kwa shughuli hiyo.
Serikali ya Kenya imeahidi kulipa gharama ya kuendesha Kesi hiyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :