Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 kuwazawadia wadau wake
Posted in
No comments
Tuesday, July 10, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Mt.
Kilimanjaro Marathon 1991 taasisi inayoendesha mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon
itawazawadia wadau waliofanikisha mbio za mwaka 2012 ambazo zilipambwa na
mlimbwende na mcheza sinema maarufu kutoka Marekani Deidre Lorenz.
Mbio
za Mt. Kilimanjaro Marathon mwaka huu zilishughudia wakimbiaji kutoka nchi
mbalimbali zakiongezeka na kuzifanya kuendelea kuwa mbio zinazopendwa na
wakimbiaji wasio na ujuzi wa kukimbia (Fun Run)!
Mbio
za mwaka huu zitakumbukwa kwa mambo matatu makubwa.
Mosi ni ujio wa mblimbwende na mcheza
sinema maarufu Deidre Lorenz kutoka katika jiji la mapesa la New York City au
linavyojulikana kama “The Big Apple”
Lorenz
anayemiliki kampuni yake mweneywe ya kutengeneza filamu ya Thira Films LLC
alidhihirisha kwa vitendo uchangiaji wake wa kuutangaza mlima Kilimanjario kuwa
ni mali ya asili ya taifa letu.
Ujio
wa Lorez aliyekwisha kucheza filamu nyingi zikiwamo Santorini Blue, The Big
Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi kulileta hamasa kubwa kwenye mbio
za marathon.
Jambo
la pili ni zawadi ya kukimbia kilometa 50 ambayo Chris Wilde aliyoipatia
Tanzania kwa ajili ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Wilde
mganga msaidizi kutoka katika jiji la Minnesota alikimbia mbio hizo kwa kila
kilometa iliwakilisha mwaka mmoja wa uhuru.
Mkimbiaji
huyo kijana aliahidi kuja tena Tanzania kukimbia kilomta 51 mwakani
kusheherekea miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika pamoja na miaka 23 ya kuanzishwa
kwa Mt. Kilimanjaro marathon mwaka 1991.
Jambo
la tatu kubwa ni mbio za Mt. Kilimanjaro kutimiza miaka 22 tangu zilipoanzishwa
na Marie Frances mwaka 1991. Frances mkazi wa jiji la matajiri la Bethesda
lililoko nje kidogo ya jiji la Washington DC nchini Marekani.
Kuzawadiwa
kwa wadau waliochangia kufanikisha mbio hizi ni mkakati wa Mt. Kilimanjaro
Marathon 1991 kujipambanua kama taasisi inayojali na kusheshimu uchangiaji wa
kuiendeleza tasnia ya riadha. Hii ni mara ya kwanza kwa tasisi ya michezo kutoa
zawadi kwa wadau walioichangia katika kufanikisha melengo yake!
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :