WATUHUMIWA WALIOKAMATWA KWA KUTAKA KUMUUA ALBONO WAACHIWA HURU
Posted in
No comments
Tuesday, July 10, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
MTOTO
Mlemavu wa Ngozi (Albino) Adam Robert (13) wakati akiwa amelazwa
hospitalini baada ya kujeruhiwa na kwa kukatwa mkono na kisha
kunyofolewa Vidole sita vya mikono yote miwili,picha hii ilipigwa siku
moja tu baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,Picha
hii ilipigwa Oktoba 14 mwaska 2011.
HUYU ndiye baba mzazi wa Adam ambaye alidaiwa kuhusika katika tukio la kujeruhi mwanaye ambaye ni Albino,ambaye anadaiwa alikuwa umbali wa hatua 3 kutoka alipokuwa akikatwa mwanaye lakini hakufanya jitihada zozote za kumuokoa,hapa akiwa na pingu chini ya ulinzi mara baada ya kutiwa mbaroni.
MLEMAVU wa ngozi Mtoto Adam akiwa hospitalini baada ya kupona majeraha yake aliyokatwa na kujeruhiwa vibaya.(Picha zote na David Azaria Geita yetu).
WATUHUMIWA watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kujaribu kumuua Mtoto Mlemavu wa Ngozi Albino Adam Robaert (13) katika mahakama ya wilaya ya Geita, wameachiwa huru na sasa wamerejea nyumbani wakiendelea na maisha yao ya kawaida.
HUYU ndiye baba mzazi wa Adam ambaye alidaiwa kuhusika katika tukio la kujeruhi mwanaye ambaye ni Albino,ambaye anadaiwa alikuwa umbali wa hatua 3 kutoka alipokuwa akikatwa mwanaye lakini hakufanya jitihada zozote za kumuokoa,hapa akiwa na pingu chini ya ulinzi mara baada ya kutiwa mbaroni.
MLEMAVU wa ngozi Mtoto Adam akiwa hospitalini baada ya kupona majeraha yake aliyokatwa na kujeruhiwa vibaya.(Picha zote na David Azaria Geita yetu).
WATUHUMIWA watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kujaribu kumuua Mtoto Mlemavu wa Ngozi Albino Adam Robaert (13) katika mahakama ya wilaya ya Geita, wameachiwa huru na sasa wamerejea nyumbani wakiendelea na maisha yao ya kawaida.
Kwa
mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Gazeti hili watuhumiwa
hao wakiwemo wazazi wa Mtoto huyo Robert Tangawizi, waliachiwa huru
tangu Mei 30 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi kutokana na amri kutoka
kwa Mwendesha mashitaka mkuu wa serikali Elieza Feleshi.
Watuhumiwa
walioachiwa huru kwa amri hiyo ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa serikali
ni pamoja na Baba wa Mlemavu huyo Robert Tangawizi,Mama wa Kambo Agnes
Majala,pamoja na mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji
Machibya Alphonce wote wakazi wa kijiji cha Nyaruguguna kata Tarafa na
Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita.
Washitakiwa
hao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na mashitaka mawili kila mmoja
katika mahakama hiyo ya wilaya,ambayo ni pamoja na Kujaribu kuua,pamoja
na kula njama ya kutaka kuua,ambapo walikamatwa Oktoba mwaka 2011 na
baada ya mahojiano na polisi walifikishwa katika mahakama hiyo ya
wilaya.
Inadaiwa
kuwa kukamatwa kwa watuhumkiwa hao kulitokana na maelezo ya mtoto
mmelavu aliyejeruhiwa ambaye alidai kuwa siku ya tukio baba yake mzazi
alimkaribisha mtuhumiwa anayedaiwa kumkata na kumjeruhi pamoja na kwamba
mtoto huyo tayari alikuwa amekwishatoa taarifa za mtuhumiwa huyo kwamba
alikuwa akimfuatilia machungani na kumdanganyadanganya.
Alieleza
kuwa hata baada ya kukataa kula mtuhumiwa huyo na kuamua kwenda kuulala
ndani ya nyumba baba yake aliendelea kumuita na kumtaka kubebea chakula
kupeleka ndani na wakati akiwa njiani kupeleka chakula ndipo
alipovamiwa na kuanza kukatwa mapanga huku baba yake akishuhudia kwa
macho,na wakati huo mama yake wa kambo alikuwa akimmulika kwa tochi.
Uchunguzi
umebaini kuwa serikali kupitia Mwendesha Mashitaka wake Mkuu imeonesha
nia ya kutoendelea na mashitaka dhidi ya watuhumiwa hao
(NOLLE-PROSECUI), ambayo hutolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 91 kifungu
kidogo cha kwanza cha Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya jinai sura ya
20 ya mwaka 2000.
Kwa
mujibu wa kifungu hicho Mwendesha mashitaka Mkuu wa serikali (DPP)
anayo mamlaka ya kutoa maamuzi ya kumuachia huru mshitakiwa yeyote na
kwa wakati wowote, endapo ataona kuna haja ya kufanya hivyo bila
kuhojiwa na mtu yeyote.
Uchunguzi
zaidi umebaini kuwa Barua ya kuachiwa kwa watuhumiwa hao (Nolle
Prosecui) ilisainiwa Aprili 28 mwaka huu na T. Vitalis ambaye ni
Mwanasheria wa Serikali mkuu, na kusomwa katika mahakama hiyo ya wilaya
Mei 30 mwaka huu na siku hiyo hiyo washitakiwa hao waliachiwa majira ya
saa 4 asubuhi.
Kwa
mujibu wa maelezo ya awali ya Mwendesha mashitaka wa polisi katika
mahakama hiyo ambayo ilianza kusomwa katika mahakama hiyo Oktoba 24
mwaka 2011 katika mahakama ya wilaya ya Geita mbele ya hakimu Mwandamizi
wa mahakama hiyo Zablon Kesase, ambayo haikuwahi kusikilizwa kwa
kipindi chote cha miezi minane kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na
mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa
mujibu wa maelezo hayo ya awali katika mahakama hiyo watuhumiwa hao
wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 14 mwaka jana majira ya saa 1:30
katika kijiji cha Nyaruguguna Kata ya Nyang’hwale,ambapo walimkata mkono
Mtoto Adam na kisha kumnyofoa vidole sita vya mikono yote miwili.
Kwa
mujibu wa Mwendesha mashitaka wa polisi Thomas Mboya watuhumiwa hao
walidaiwa kuhusika katika tukio la kumjeruhi Mlemavu huyo kwa lengo la
kukata na kunyofoa baadhi ya viungo vyake na kutoweka navyo na
kumsababishia kilema cha maisha.
Mlemavu
huyo alilazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa miezi miwili na
baada ya kupona alikataa kutoka katika hospitali hiyo ya wilaya kwa
ajili ya kurejea nyumbani kwao kijijini kwa hofu ya kuuawa na watu
waliomkata na kumnyofoa vidole vyake.
Hali
hiyo ilimfanya Mlemavu huyo kukaa katika hospitali hiyo kwa miezi
miwili kabla ya kujitokeza wasamaria wema waliomchukua na kwenda kuishi
naye Jijini Dar es Salaam, na hiyo ni baada ya Gazeti hili la Habari Leo
kuandika habari nyingi pamoja na makala zilizohusu Madhila ya Mlemavu
huyo.
Baadhi
ya wananchi pamoja na wapigania haki za binadamu wameonesha kustushwa
na kuachiwa na watuhumiwa hao,kwa madai kuwa hatua iliyochukuliwa na
Mwendesha mahitaka Mkuu wa Serikali ya kutia sahihi kwa niaba ya Jamhuri
kutokuwa na nia ya kuendelea na Mashitaka jalada la watuhumiwa imekuwa
ya haraka tofauti na matarajio ya wengi.
Walidai
kutokana na vitendo vya mauaji na kujeruhiwa kwa watu wenye ulemavu wa
Ngozi (Albino) kuonekana kurejea kwa mara nyingine tena nchini,hakukuwa
na sababu zozote za msingi za kuwaachia watuhumiwa hao kwa haraka,hali
ambayo walidai inachochoea mauaji dhidi ya walemavu hao kutokana na
sheria kutokuwa na makali.
Paulina
Alex ni mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu ambaye pia ni
Mkurugenzi wa shirika la NELICO ambalo ni miongoni mwa mashirika
yanayojihusisha na utoaji wa mafunzo kuhusiana na haki za binadamu,
unyanyapaa, huku akiishi na baadhi ya walemavu wa ngozi wasiokuwa na
wazazi pamoja na wala wanaoishi katika mazingira magumu, anasema ni
lazima serikali iwe na sheria kali kuhusiana na watu wanaojihusisha na
mauaji ya Albino.
Akizungumzia
kuachiwa kwa watuhumiwa hao Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Geita Desdery
Kamugisha alisema wao kama mahakama hawana mamlaka ya kulazimisha
kuendelea kusikiliza kesi ambayo Mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali
(DPP) asmeamuaru kufutwa ama kuachiwa kwa watuhumiwa.
“Mwendesha
mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anayo mamlaka ya
kutoa maamuzi ya kumuachia mshitakiwa yeyote Yule ambaye anakabiliwa na
mashitaka ya aina yoyote,na anatoa maamuzi hayo chini ya kifungu 91(1)
cha sheria ya mwenendo wa mashitaka ya jinai sura ya 20 ya mwaka 2000,na
katika hilo hairuhusiwi mtu yeyote,na anayo mamlakaa ya kutotoa sababu
za kufanya hivyo…….kwa hiyo sisi hatuna mamlaka tena ya kuhoji hilo na
ndiyo maana tumetekeleza amri na kuwachia…..’’ alifafanua Hakimu
Kamugisha.
Hata
hivyo kifungu hicho kinachotumiwa na Mwendesha mashitaka Mkuu wa
serikali (DPP) na kuwaachia watuhumiwa kimekuwa kikilalamikiwa kwa muda
mrefu na wadau wa haki za binadamu kwa madai kuwa kimekuwa kikisababisha
hata watu wenye mahitaka stahili kuachiwa na hivyo kuaondoa dhana ya
Utawala Bora,lakini hakuna hatua zozote zambazo zimekwishachukuliwa
katika kurekebisha ama kujadili kifungu hicho na kukifanyia
marekebisho.
Habari na David Azaria, wa Geita yetu
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :