WATUHUMIWA WA NOTI BANDIA MBARONI KILIMANJARO
Posted in
No comments
Monday, July 23, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
JESHI la polisi Mkoani Kilimanjaro, limekamata Noti Bandia
za sh. 10,000 zenye Thamani ya sh. 600,000 fedha za Kitanzania na kushikilia watuhumiwa
wawili katika tukio hilo lilitokea katika maeneo ya kituo cha petroli cha Karanga,
Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi kwa vyombo vya habari, Watuhumiwa
hao Husna Karimu(36) ambaye ni mkazi wa Majengo-Dar es salaam na Hamza Mohamedi
(60), Mkulima, Mkazi wa Mijongweni, Mkoani Kilimanjaro, walifika dukani kwa
Sharifa Saidi ambaye ni mfanyabiashara wakihitaji kupewa huduma ya kutuma pesa
kwa njia ya M-pesa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa upelelezi
mkoani Kilimanjaro, Ramadhani Ng’anzi, alisema kwamba watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 21 julai mwaka
huu, wakiwa na noti 22 za Tshs. 10,000 zenye namba BF1547948 na Noti 17 za
Tshs. 10,000 zenye namba BC2937831.
Alisema kwamba, Mtuhumiwa wa kwanza ambaye ni Mkazi wa
Majengo Jijini Dar es salaam, mpaka sasa haijafajhamikka mara moja shughuli maalum
iliyomleta mkoani hapo lakini uchunguzi zaidi unaendelea na mara baada ya
kupata vielelezo kamili, hatua za kisheria zitafuta mkondo wake ikiwa ni pamoja
na kuwafikisha Watuhumiwa hao Mahakamani.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro lilitoa tahadhari
kwa Wananchi hasa Mawakala wa Makampuni ya Simu za mkononi kwa njia ya Mtandao
wa Makampuni hayo kwamba kuna Wimbi la utoaji wa Noti za Bandia, hivyo wawe
makini na kushirikiana na Vyombo vya Usalama katika kuhakikisha wimbi la Matukio
kama hayo yanayoanza kujitokeza yanakomeshwa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :