Waziri Maghembe atangaza neema ya maji nchini
Posted in
No comments
Tuesday, July 10, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
SERIKALI imetangaza neema ya kukabiliana na uhaba wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na makao makuu ya mikoa nchini.
Kauli hiyo, ilitangazwa jana bungeni mjini hapa na Waziri wa Maji,
Profesa Jumanne Maghembe, alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya
Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2012/13, ambapo alisema utekelezaji wa
mpango wa dharura utasaidia kuondoa hali hiyo.
Alisema yupo
katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuboresha huduma ya maji
katika Jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo.
Alisema
mpango huo, unalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa maji kutoka mita
za ujazo 300,000 kwa siku kwa sasa hadi mita za ujazo 710,000 kwa siku
ifikapo mwaka 2014.
Akizungumzia
upanuzi wa mradi wa maji wa Ruvu Juu, alisema Mhandisi Mshauri,
ameshaanza kazi ya usanifu wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu na bomba kuu
la maji linalotoka Mlandizi Pwani hadi Kimara, Dar es Salaam, tangu
Machi, mwaka huu.
Alisema upanuzi wa mradi huo, utasaidia
kuongeza uwezo wa mtambo kutoka mita za ujazo 82,000 kwa siku hadi mita
za ujazo 196,000 kwa siku, ili kukabiliana na ukuaji wa miji ya
Mlandizi, Kibaha na Dar es Salaam.
Alisema chini ya utekelezaji
wa mpango huo, Serikali itaimarisha miundombinu, inakabiliana na
ongezeko la watu na pia inahakikisha maji yanapatikana kwa wingi,
ikiwamo wakati wa kiangazi ambapo maji ya Mto Ruvu hupungua.
Kuhusu
mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Kahama, Shinyanga, alisema
Serikali imeendelea kuusimamia ambapo upatikanaji wa maji katika mji wa
Shinyanga na Kahama, umeongezeka.
Kwa mujibu wa Profesa Maghembe,
upatikanaji wa maji katika mji wa Shinyanga, umeongezeka kwa kuwa
wanaopata maji ni wateja 13,827, ikilinganishwa na wateja 13,117
waliokuwa wakipata maji Machi, mwaka huu.
Kwa upande wa mji wa
Kahama, alisema wanaopata maji ni wateja 8,856 waliokuwa wakipata huduma
hiyo Machi, mwaka huu, ikilinganishwa na wateja 8,308, waliokuwa
wakipata maji mwaka jana.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :