Waziri wa Mawasiliano Z’bar ajiuzulu

Posted in
No comments
Tuesday, July 24, 2012 By danielmjema.blogspot.com



WAZIRI wa Miundombinu na Mawasiliano,Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake jana. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Masoud kujiuzulu.

“Julai 20,2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,.Dk. Ali Mohammed Shein ya kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit, iliyotokea Julai 18,2012,” ilisema taarifa hiyo.

Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Dk. Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani(CUF), Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa mpya wa Miundombinu na Mawasiliano.

“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kushika wadhifa huo,” taarifa ya Ikulu ilisema.

Wakati huo huo, Dk. Shein ameunda tume kwa ajili ya ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit.

Tume hiyo, inaongozwa na Mwenyekiti Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kapteni Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .