Yanga na APR zafuzu
Posted in
No comments
Tuesday, July 24, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Klabu bingwa mtetezi Afrika
Mashariki na Kati, Yanga ya Tanzania, imefanikiwa kuingia nusu fainali
ya mashindano ya Kombe la Kagame baada ya kuitoa timu ya Mafunzo ya
Zanzibar kwa mikwaju ya penalti.
Matokeo hadi mwisho wa mchezo mjini Dar es
Salaam siku ya Jumatatu yalikuwa 1-1, Mafunzo wakiwa wa kwanza kupata
bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Ali Mmanga.
Yanga
walifanikiwa kusawazisha dakika ya kwanza kipindi cha pili kupitia kwa
Said Bahanuzi na kufanya mchezo uamuliwe kwa penalti baada ya dakika
tisini, na Yanga kushinda kwa penalti tano kwa nne.
Yanga watacheza na APR ya Rwanda, ambao nao wametinga nusu fainali baada ya kuwatoa URA wa Uganda kwa mabao 2-1.
APR walipata mabao yao kipindi cha kwanza
kupitia kwa Jean Claude Iranzi na Seleman Ndikumana, wakati bao la URA
lilifungwa na Robert Ssentongo kipindi cha pili.
Kocha wa APR Mholanzi Ernest Bradnt anasema
itakuwa mechi ya kulipiza kisasi; “Yanga walitufunga hatua ya makundi,
hivyo tutahitaji kulipiza kisasi. Lakini pia tumeshinda kombe hili mara
tatu nyumbani na sasa tunataka kulishinda ugenini, hapa Tanzania,”
alisema.
Jumanne Simba itacheza na timu mpya kwenye
mashindano haya, Azam, pia kutoka Tanzania, na Vita Club ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo itacheza na Atletico ya Burundi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :