BREAKING NEWS:Mafuriko yauwa watu 35 Nigeria!!!
Posted in
No comments
Tuesday, July 24, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Watu wapatao 35 wamekufa
kufuatia mafuriko yaliyotokea katikati mwa Nigeria baada ya mvua kubwa
na kusababisha bwawa kufurika karibu na mji wa Jos.
Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika
eneo hilo amesema nyumba zipatazo mia mbili, nyingi zikiwa zimejengwa
kwa udongo zimezama au kuharibiwa na mafuriko.
Maafisa wanasema watu wapatao ishirini na watano hawajulikani walipo na kwamba idadi ya watu waliokufa inatarajiwa kuongezeka.
Shirika la Taifa la Kushughulikia Majanga limeanza operesheni ya misaada ya dharura.
Mtu mmoja alinukuliwa akisema kuwa amewapoteza watoto wake saba katika mkasa huo.
Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika Jimbo la Plateau amesema miongoni mwa waliofariki ni mzee wa miaka 90
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :