MUINGEREZA KUONGEZA NGUVU TIMU YA UTETEZI KESI YA RUFAA YA SAGAHUTU
Posted in
No comments
Tuesday, July 24, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imemruhusu mshauri wa masuala ya sheria wa Uingereza, Wayne Jordish kuongeza nguvu katika timu ya utetezi wakati wa kusikiliza rufaa ya afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda, Kapteni Innocent Sagahutu.
‘’Ushiriki
wa Jordish wakati wa kusikiliza rufaa utakuwa na manufaa kwa Sagahutu
na utasaidia Mahakama ya Rufaa kuelewa kwa undani hoja za rufaa,’’
Majaji wanaeleza katika uamuzi wao na nakala yake kupatiwa Shirika la
Habari la Hirondelle Jumatatu.
Kwa
mujibu wa uamuzi huo, Jordish atazungumza mbele ya mahakama hiyo na
kutoa ushauri kwa timu ya utetezi ya Sagahutu bila kudai malipo yoyote
kutoka mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wengine katika timu ya utetezi ya Sagahutu ni pamoja na Wakili Kiongozi, Fabien Segatwa na Msaidizi
wake Scott Martin. Tarehe ya kusikiliza rufaa hiyo bado haijapangwa.
Katika
rufaa yake, Sagahutu anapinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya awali
Mei 17, 2011katika kesi ijulikanayo kama Military II, akishitakiwa
katika kesi moja na maafisa wenzake watatu ambao ni pamoja na Majenerali
wawili, Augustin Bizimungu na Augustin Ndindiliyimana na Meja
Francois-Xavier Nzuwonemeye.
Wote
walitiwa hatiani kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.
Wakati Bizimungu alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, mwenzake,
Ndindiliyimana alihukumiwa adhabu ya muda aliokwishatumikia tangu atiwe
mbaroni Januari 29, 2000. Nao Nzuwonemeye na Sagahutu walipewa adhabu ya
kutumikia miaka 20 jela kila mmoja wao.
Jordish
alishawihi kuwa katika timu za utetezi katika kesi mbili tofauti ICTR
ikiwa ni pamoja na ya Meya wa zamani wa Rwanda, Ignace Bagilishema
ambaye aliachiwa huru na Michael Bagaragaza ambaye ameshahitimisha
kutumikia adhabu yake ya kifungo cha miaka minane jela.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :