Global Publishers Nao Walalamikia Tuzo Za Blogers Za Vodacom

Posted in
No comments
Thursday, August 2, 2012 By danielmjema.blogspot.com


Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Vodacom kwa kuja
na wazo zuri la kutambua michango na umuhimu wa mitandao ya kijamii,
hususan blogs na web site na kuamua kuwatunuku.

Pamoja na pongezi hizo, lakini mmekosea katika utekelezaji wake. Kwa
mtizamo wa wahusika wengi (Blogers), tuzo mlizotoa baadhi zimeenda kwa
wasiostahili na mmeacha wengi waliostahili kupata tuzo hizo.

Ingawa hamkuweka wazi vigezo vyote, lakini baadhi ya mlivyovitaja ni
pamoja na blog kuwa inayofanyakazi (active), ambayo inaweka habari
mpya kila siku, iwe inayoandika vitu halisi na siyo vya kukopi au
kutafsiri kutoka BBC na mitandao mingine ya Kiingereza na kupesti.

Hali kadhalika mkasema kuwa web site au blog hiyo inachokiandika kiwe
kimeandikwa na mtu mwenye ujuzi nacho, mkatoa na mfano kuwa kama ni
mapishi, basi yaandikwe na mtu mwenye kujua mapishi. Pia mtandao huo
uwe maarufu.

Bila shaka kwenye ulimwengu wa mitandao, unaposema mtandao fulani ni
maarufu, ina maana unatembelewa na visitors wengi kwa siku, mtandao
hauwezi kuwa maarufu kisha ukawa na visitors 500 au 800 tu kwa siku.

Bloggers maarufu nchini wanajuana na wanahesabika, inakuwa kichekesho
inapokuja kutangazwa blog fulani ndiyo maarufu wakati haijulikani hata
miongoini mwa bloggers wenyewe, achilia mbali wasomaji wengine.

Hawa ndiyo washindi wenyewe:
-Mikocheni Report,
-Issa Michuzi
-Wanamuziki Tanzania.
-Kipanya.co.tz
-Vijana FM
-Millardayo.com
-Taste of Tanzania
-Jamii Forums
-Mambo Magazine
-DJ Fetty Blog

Kwa mtizamo wa wengi, katika orodha hiyo ya watu kumi, ni wanne tu
ndiyo walistahili na waliobaki hawakustahili kabisa, kwa sababu licha
ya kuwa hawajulikani sana, lakini pia huoni hata namna ambavyo
Vodacom, kama kampuni, inaweza kunufaika nao iwapo mtaamua kujitangaza
kupitia kwao.

Kuna Bloggers wameachwa ambao wao ku blog ndiyo maisha yao, wanalala,
wanaamka, wanatembea, wanakula, wanakunywa, wanakaa wana blog tu. Wao
na Blog, Blog na wao. Hakuna taarifa, breaking news au picha za
matukio yote muhimu zinazowapita hapa nchini na hata katika kuripoti
matukio ya promosheni ya Vodacom kwenye mitandao yao wako mstari wa
mbele. Wengine kazi yao ni kukopi na kupesti kazi za wengine!

Pengine hatuyajui malengo ya Vodacom, kwa sababu kama kweli mnanataka
kuthamini michango ya 'social media' na wao kunufaika na media hizo,
basi mmekosea katika hili.

Waulizeni mliowatuma, wamefanya research ya kutosha na kuona hao
washindi wana visitors wangapi na pageviews ngapi kwa siku? Je, Google
Analytics Report zao zinaoneshaje? Na, je, habari na picha
wanazoziweka kwenye mitandao yao, kweli ni za kwao, au wamekopi na
kupesti tu kutoka kwingine?

Naomba mliopewa kazi ya kuandaa tuzo hizi myachukue haya kama
changamoto na kuyafanyia kazi ili msiharibu kazi nzuri inayofanywa na
Vodacom nchini Tanzania na wala hatuyasemi haya kwa sababu ya chuki
binafsi, bali kwa ukweli na uwazi tu!

Wassalaam!
Global Publisherstz.com

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .