Rais Kikwete: madai ya walimu hayalipiki

Posted in
No comments
Thursday, August 2, 2012 By danielmjema.blogspot.com


Rais Jakaya Kikwete akilihutubia taifa kupitia wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jana Ikulu mjini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.

HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete, amevunja ukimya na kuasema madai ya walimu ya kushinikiza kupandishiwa mishahara kwa asilimia 100 hayawezi kutekelezeka.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete, imekuja siku chache tangu Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), kutangaza mgomo wa nchi nzima ambao unaendelea katika mikoa mbalimbali.

Akihutubia taifa katika utaratibu wake, alijioweka kila mwisho a mwezi kupitia Wahariri vyombo mbalimbali vya habari, Ikulu mjini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete, alisema uwamuzi huo unatokana na Serikali kutokuwa na uwezo wa kulipa kiasi hicho kinachoshinikiwa na walimu.


“Hili la waalimu sitaki kulizungumzia sana, kwa sababu liko mahakamni na kesho (leo), uwamuzi utatolewa, lakini walau naona niseme kidogo tu …., kwa muda mrefu tulikuwa na mazungumzo na walimu na madai yao yalikuwa kupandishiwa wa mshahara kwa asilimia 100, posho ya walimu wanaofundisha masomo ya sayansi asilimia 55, posho ya mazingira magumu asilimia 30 pamoja na posho ya kujikimu kwa asilimia 50.

“Ingawa jambo hili lipo mahakamani, labda niseme kidogo kuhusu ufafanuzi juu ya madai ya walimu wetu na vema basi wakaepuka kutumia watoto katika maandamano yao kama njia ya kufikisha ujumbe wao.

“Tunajua hivi sasa maana kuna taarifa zinaeleza baadhi ya walimu ambao hawataki kushiriki mgomo kwa kuona hawawatendei haki watoto, sasa wale wanaoshirikia nasiki wanapigwa na kuzomewa, nasema kwa hili hapana ndugu, wanaotaka kufanya acheni wafanya kazi.

“… yote haya kama utaamua kuyafanyia kazi kwa upande wetu Serikalini hatuwezi kutekeleza kwa sababu hatuna uwezo wa kulipa,

“Na haya tumekuwa tukielezana na walimu muda mrefu, lakini wakati sisi tukieleza ukweli wenzetu wakaamua kutoka na kwenda Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na hata tulipofika kule tulisema haya haya.

“Tukiwa katika majadiliano kule CMA, tulishanga siku ya Ijumaa Julai 20, mwaka huu wakaleta barua ya mgomo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, lakini pamoja na haya siku iliyofuata ikawa ni mapumziko ambako Serikali isingeweza kufanya kazi yoyote.

“Kwa hali hii, kama utachukua madai yao na kuyafanyika kazi, Serikali italazimika kutumia Sh trilioni 6.5 kwa ajili ya mishahara pekee ya walimu… mapato yetu ya ndani ni Sh trilioni 8. kwa hesabu hizo utajikuta kwa mwaka unatumia fedha kulipa mishahara ya wafanyakazi na Sh trilioni 2 ndizo unaweza kuzipeleka katika huduma za jamii… tunasema hili hapana.

“Na kama tutajaribu kufanya hivi kuna hatari kwa Serikali yetu, ikawa ya ajabu kwa kulipana mishahara sisi peke yetu. Kubwa ninawaomba sana nitakuwa mtu wa mwisho kuwadharau walimu, kwani ninatambua mchango wao katika aifa letu.

“Hata nami nilipofika hapa ni mchango mkubwa wa walimu, ila kwa hili wanalotaka la nyongeza madai yao sioni uwezo wa kupata fedha hizi na kama tukijaribu kufanya hivi kuna hatari ya nchi yetu kushuhudia maandamano ya wananchi kupinga matumizi ya kulipana mishahara kwa watumishi 500,000 wa Serikali waliopo sasa,” alisema Rais Kikwete.

Sakata la Dk. Ulimboka

Akizungumzia sakata la kutekwa nyara na watu wasiliojulika kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania Dk. Stephen Ulimboka, Rais Kikwete, alisisitiza Serikali kutohusika na tukio hilo.

“Unajua linapotokea jambo lolote huwa kuna tafsiri nyingi na mengi yataandikwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu tukio hili. Tangu awali tunajua kuwa Dk. Ulimboka hakuwa mtumishi wa hospitali wa Serikali lakini tulikuwa naye katika mazungumzo na hata kukubaliana baadhi ya mambo.

“Na kama kuna mtumishi au kiongozi wa Serikali alifanya tukio hili eti kwa minajili ya kuifurahisha serikali sijui alifanya ili iwe nini. Na kama jambo lingekuwa katika vyombo vya kisheria ni vema sasa vyombo vya habari vikaruhusiwa kuchapisha barua ya madai ya madaktari juu ya nyongeza ya mishahara.

“Maunzumzo ya Serikali ya madaktari yalivunjika katika kipengelea kimoja cha madai ya mishahara ya juu na kama kuna watu wanadai eti Tscani inadhamani kama gari la VX ana aje hapa tutampatia fedha ili aende akatuletee.

“Thamani ya mashine ya T-scan moja ni Dola za Marekani 700,000 na ninapenda niweke wazi tangu nilipongia madarakani tumeweza kuboresha sekta ya afya ambayo awali.

“Awali bajeti ilikuwa Sh bilioni 271, lakini kila mwaka tumekuwa tukiiongeza hadi kufikia Sh trilioni 1.2 huku kila hospitali ya mkoa ikifanyiwa marekebisho makubwa sambamba na vipimo vya magonjwa,” alisema Rais Kikwete.

Ajali ya Meli

Akizungumzia jail ya meli ya MV Skagit, iliyotokea Julai 18 mwaka huu, Rais Kikwete, alizitaka mamlaka zinahusika kuwa na utaratibu wa kikomo cha matumizi ya meli hizo.

“Ninapenda kulieleza taifa kuwa hivi sasa Sumatra pamoja na Mamlaka ya meli Zainzibar zinafanya kazi kwa pamoja kwa kuitumia taasisi ya chuo ubaharia ya DMI, kama mshauri mwelekezi katika usajili na matumizi ya meli.

GESI

Kuhusu suala la gesi, Rais Kikwete alisema Serikali imepata mafanikio makubwa ambayo yataifanya Tanzania iwe moja ya nchi zinazozalisha gesi kwa wingi.

“Napenda kuwaambia kwamba juhudi za kutafuta mafuta zilianza mwaka 1952 ambapo vilichimbwa visima na Kampuni ya Shell BP, lakini hakuna mafuta wala gesi iliyopatikana,

…. Kuanzia mwaka 1954 mpaka mwaka huu jumla ya visima 51 vya mafuta vimechimbwa na kati ya hivyo visima 22 vimekutwa vinatoa gesi asili vimegundulika visima 8 baharini na 12 nchi kavu katika mikoa ya Mtwara, Pwani na Lindi,

“Haya ni mafanikio makubwa ambayo tunaweza kujivunia, kama tukiendelea hivi tunaweza kuzalisha na kuwa na akiba ya futi za ujazo trilioni 25.4 mpaka 28.9 hivi, napenda kuwahakikishia Watanzania kwamba yapo matumaini makubwa ya kupata gesi na mafuta,

…tumezungumza na wakubwa hawa, wamewekeza, kama tukifanikiwa hivi, ni wazi Tanzania inaweza kuwa nchi ya kutumainiwa duniani,

Alisema pamoja na kupata mafanikio hayo makubwa, Serikali inakabiliwa na changamoto nyingi.

“Moja ya changamoto ya kwanza inayotukabili sasa ni kujenga uwezo wa kushibiti kampuni zinazofanya kazi ili kupata malipo yanayostahili… nasema hivi kwa sababu hapa kutakuwa na wajanja wajanja lazima tuwabane,

…tunatakiwa kuzalisha watalaamu wazalendo ambao watasimamia eneo hili vizuri, tunapaswa kuwa na wahasibu, wakemia, mainjinia katika maeneo yote ya Mnazi Bay na Songo Songo… hii ni mali ya Serikali,

“Nasema tusipojenga uwezo wa watu tutakuwa na hatari ya kudhulumiwa hapa….kwa mikakati hii tutafanikiwa,”alisema Rais Kikwete.

…tuna kila sababu ya kupata Watanzania wengi wenye uwezo ili kukwepa watalaam, vinginevyo tutajikuta wao ndiyo wanafaidi kuliko wazawa… majibu yote ya haya yapo kwenye elimu ya Sayansi na Hisabati.

Alisema lazima shule za msingi, vyo na sekondari vianze kufundisha masomo, vikiwemo Chuo Kikuu cha Nelson Mandela (Arusha), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) , Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), DIT Mbeya na mikoa mingine.

Alisema changamoto ya pili ni namna ya kudhibiti mapato yote yakayopatikana ili yatumike vizuri kwa manufaa ya Watanzania, kwa sababu kuna weza kuwapo na watu walaghai, wajanja ambao wanaweza kunufaika.

“Ili kuepuka haya yote, lazima tubadilishe sheria za gesi ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza, hatutaki kuona tunaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe,”alisema Rais Kikwete.

UMEME

Kuhusu suala la umeme, Rais Kikwete alisema kumekuwa na tatizo la mgawo wa umeme kujirudia mara kwa mara, hali ambayo inadhoofisha uchumi wa taifa.

Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imekuwa na mipango ya kukabiliana na tatizo hilo.

Kuhusu uwamuzi wa kuligawanya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Rais Kikwete alisema Serikali imeshindwa kuligawa shirika hilo kutokana na kiwango kidogo cha umeme kinachozalishwa.

“Kweli kwa muundo namna ulivyo shirika hili limekuwa kubwa na lina mambo mengi, lakini tumeshindwa kutenganisha majukumu yake kutokana na kiasi cha umeme unaozalishwa ni mdogo… sasa kweli uzalishaji Megawati 400 halafu ugawe kwa makampuni matatu haiwezekani,”alisema Rais Kikwete.

RUSHWA

Kwa upande wa rushwa, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema Serikali inaendelea na vita dhidi ya wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

“Rushwa bado ipo kweli si uongo, zile kubwa na ndogo, lakini tumefanya kazi kubwa ya kuzijengea uwezo taasisi zinazohusika, kwani mpaka sasa kesi kubwa 30 zipo mahakamani,”alisema Rais Kikwete.

CHENJI

Kuhusu rushwa ambayo ilighubika ununuaji wa rada miaka cada iliyopita, Rais Kikweye alisema ni vigumu watu wanaotuhumiwa kushitakiwa, kwa sababu Kampuni BAE System ya Uingereza imeshindwa kushibitisha kama kulikuwa na rushwa wakati wa ununuzi.

“Nililetewa ujumbe na Waziri Mkuu wa Uingereza hapa ofisini kwangu, niliiangalia vizuri na badea nilikwenda Uingereza ambako wale jamaa walitoa ufafanuzi kwamba, hakukuwa na suala la rushwa wakati wa kuuziana, bali wenyewe walikosea kuandika kwenye vitabu vyao,”alisema Rais Kikwete.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .