KIPANDE CHA WIMBO WAZUA MTAFARUKU KATI YA NEY NA MONGO MOVIE

Posted in
No comments
Wednesday, August 8, 2012 By danielmjema.blogspot.com

kipande cha wimbo wa msanii wa Bongo Fleva Ney wa Mitego ambaye anasifika kwa kuimba chochote kile anachojiskia kuimba bila kujali mapokezi ya wanaomsikiliza, kimezua mtafaruku kati yake na Bongo Movie kutokana na Bongo kuhisi wamedhalilishwa.

Hata hivyo katika utetezi wake, Msanii Ney alisema kuwa kile alichokizungumza ni cha kweli na kasma kuna mtu anahisi kaonewa ajitokeze na kukanusha madai ya Mstari wa wimbo huo.

 Ney alisema kuwa alifikia kufanya wimbo huo baada ya kufanya research ya kutosha na kusema kwamb akatika list yake kuna Wasanii watatu ambao majina yao alisema kwa sasa anayaweka kapuni ila waklimchokoza atafunguka tu.

"Kuna rafiki yangu alikua amemzimia mwanadada mmoja wa Bongo Movie sasa kilichotokea siku moja wakati tumetoka wote, tukiwa kwenye klabu moja maarufu hapa mjini, yule jamaa si akaamua kumtokea yule Staa, ila cha kushangaza yule bishosti alimwambia kwa mapenzi no ila kama ana mpunga wa kutosha atafikiria kumpa mzigo," alisema Ney na kuendelea

"Jamaa akanifuata kuomba ushauri mimi nikamwambia kama ishu ndivyo ilivyo asihofu wala nini ampe hele ili akate kiu, jama kweli mpunga anao akampa yule demu sh 500,000 na usiku uleule tukaondoka na mzigo,"alisema Ney.

Ney anasema kuwa waliamua kufanya resaerch kwa mabinti kama wawili wengine na ishu ilikuwa ni vilevile.

BONGO MOVIE WANASEMAJE?

Kwa upande wake katibu wa BONGO MOVIE CLUB Msanii Musa Issa maarufu Cloud 112, alikiri kusikia skendo hiyo kwenye Vyombo vya habari ila kama watagundua Ney hana evidence watamshitaki kwa kuidhalilisha tasnia hiyo.

SHAMSA FORD: yeye anasema kuwa huo ni ujinga na kwamba sio ishu kwa mtu kutaka kupata umaarufu kupitia kwa migongo ya wengine akisisiza kwamba wao wanafanya kazi kama kazi nyingine na wala sio kama wanajiuza.

HEMEDI PHD: "jamaa kama dizain fulani anataka maujiko vile....mimi naona tumpotezee tu huyu ni limbukeni ila kama kuna evidence poa tu"

sikiliza wimbo huo halafu unipe maoni yako kuhusu kipande hicho uanaonaje?

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .