2012 MWAKA WA MAJANGA KATIKA SANAA....KHERI YA MWAKA MPYA 2013!
Posted in
No comments
Sunday, December 30, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Marehemu Steven Kanumba
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
HII ni
Jumamosi ya mwisho kabla ya mwaka huu kumalizika na kuuanza mwaka mpya wa 2013.
Ni mwaka uliokuwa na matukio mengi katika sekta karibia zote.
Sharomillionea kabla ya umauti wake
Sio
kisiasa, kimichezo na kiutamaduni. Pande zote hizo zimeguswa na matukio ambayo
kwa kiasi Fulani yaliumiza watu na kuwaacha njia panda kwa kiasi kikubwa.
Hapa
nitaelezea japo kwa ufupi matukio ya kisanaa na burudani hasa ya vifo
yaliyotokea kwa mwaka huu, ambayo kwa kiasi kikubwa yalitikisa katika viunga
hivyo nchini.
Mariam Khamis, enzi za uhai wake
Yalichanganya
kiasi kwamba hadi sasa, ukimuuliza mtu anayefuatilia sanaa nini anakumbuka kwa
mwaka huu, ni wazi atakwambia misiba isiyopungua mitano ya wasanii wetu.
Misiba
ambayo imeacha pengo kubwa. Watu bado wanaendelea kulia na kuumizwa na misiba
hiyo. Tena misiba mingine mitatu imetokea ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ule
wa Novemba.
Tuanze na
msiba wa kwanza uliogusa watu wengi na kulifanya jiji zima litetemeke. Kila
mdau wa sanaa aliumia. Si mwingine, bali ni msiba wa Steven Kanumba, uliyotokea
nyumbani kwake Sinza Vatcan, jijini Dar es Salaam, Aprili 7.
Kifo cha
msanii huyo wa filamu hapa nchini kilihuzunisha wengi. Siku ya Aprili 8,
takribani vyombo vya habari vyote viliripoti msiba huo na kufanyia mwendelezo
katika kipindi cha zaidi ya siku 30.
Msiba huo
inadaiwa ulitokana na ugomvi wa kimapenzi kati yake na msanii mwenzake
Elizabeth Michael, maarufu kama (Lulu), ambaye hadi leo yupo rumande.
Mwili wa
Kanumba uliagwa katika viwanja vya Leaders Club, kabla ya kuzikwa makaburi ya
Kinondoni, huku msiba wake ukivunja rekodi kutokana na kujaza watu wengi.
Jiji zima
lilifurika watu. Tax zilifanya kazi pamoja na bodaboda zilizobeba watu kuwatoa
sehemu moja kwenda nyingine, hasa wale waliokuwa na haraka ya kufika eneo la
tukio.
Kwa mwaka
huu, msiba wa Kanumba ndiyo uliyokusanya watu wengi kwa mara moja, hasa
kutokana na umahiri wake katika kazi, akicheza filamu nyingi zinazopendwa hadi
leo.
Kanumba
tayari alishaanza kuvuka nje ya mipaka ya Tanzania kwa kucheza filamu zaidi ya
tatu za Kimataifa, ikiwamo ile ya Dar to Lagos.
Baada ya
msiba huo kupoa na watu kuendelea na maisha ya kawaida, mwishoni kabisa mwa
mwaka huu, msiba mwingine ulitokea katika tasnia ya taarabu, Mariam Khamis
kupoteza maisha.
Mwanadada
huyo aliyekuwa anafanya kazi na TOT Taarab, chini ya Malkia wa Mipasho
Tanzania, Khadija Omari Kopa, alifariki kutokana na matatizo ya uzazi na kuacha
kichanga.
Mwanadada
huyu alizikwa katika makaburi ya Magomeni Ndugumbi, ikiwa ni siku moja tu baada
ya kifo chake. Kutokana na imani ya dini yake ya Uislamu, mwimbaji huyo
alizikwa mapema.
Msiba wa
Mariam uligusa watu wengi katika tasnia hiyo ya taarabu, wakijitokeza watu
wengi wa kushiriki mazishi yake. Hata hivyo, bado hajaweza kufikia hata robo ya
watu waliomzika marehemu Kanumba.
Msiba wa
Mariam Khamis ulikuwa mzito kwa wadau wa taarabu hapa nchini, ukizingatia kuwa
alikuwa na mashabiki waliopenda kazi zake alipokuwa kwenye kundi hilo
linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wakati
watu wanaendelea kutafakari maisha ya sanaa na wasanii hapa nchini, wadau
walishtushwa na taarifa za msiba wa msanii wa zamani wa Kaole, Khalidi Mohamed,
maarufu kama Mlopelo, kilichotokea Novemba 23.
Msiba wa
msanii haujatingisha sana, labda ni kwasababu hakucheza nafasi zinazokaa kwenye
fikra za watu kichwani au maisha ya Kaole Sanaa Group yalivyokuwa yakishuka kwa
kasi.
Ilikuwa
hadi mtu amuelezee sana ndio mtu akumbuke sura yake au kumuona kwenye picha
yake. Hata hivyo pengo lipo, maana kila mtu ana umuhimu wake katika jamii.
Msiba wa
Mlopelo bado ukiwa mbichi, taarifa za kifo cha John Maganga nazo zilisikika na
kuzidi kuwaacha watu kwenye maswali mengi wakiangalia namna gani habari hizo
zinakuwa nyingi kwa wasanii.
Taarifa
za kifo cha Maganga zilichanganya watu wengi, tangu Novemba 25, wakipishana
siku moja, ukingatia kuwa msiba huo ingawa haujafikia mshtuko wa Kanumba, ila
wengi walimjua na kuheshimu kazi zake za sanaa hapa nchini.
Moja ya
kazi aliyocheza marehemu Maganga ni ile ya Mrembo Kikojozi iliyofanya vyema
katika tasnia hiyo ya filamu Tanzania.
Maganga
alizikwa makaburi ya Kinondoni, lakini siku aliyokuwa anazikwa, mwingine
ulitokea, huu ukiwa mkubwa zaidi kwa wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla.
Msiba huu
ulikuwa ni wa Hussein Mkiety, maarufu kama Sharomillionea, uliyotokea Novemba
27 mwaka huu. Kijana aliyeibadilisha kabisa soko la sanaa ya vichekesho. Wengi
walizoea kuigiza wamevaa vinyago.
Lakini
ujio wake ukawa na matunda zaidi. Mwonekano wake wa usafi zaidi, lakini bado
alichekesha. Ni kazi nzuri. Marehemu Sharomillionea alikufa kwa ajali ya gari
wilayani Muheza na kuzikwa katika makaburi ya kijiji chao cha Lusanga, wilayani
humo.
Ukitaka
kupanga misiba iliyogusa hisia za wengi, basi huu wa Kanumba ulishika nafasi ya
kwanza na Sharomillionea akishika namba mbili, ingawa utaratibu huu ni mchungu
zaidi, maana kiubinadamu huwezi kufananisha kupendeza kwa misiba.
TAIFA LETU.com iliwakilishwa na kijana wetu, Kambi Mbwana, ambaye pia ni mmiliki wa Handeni kwetu blog katika mazishi ya msanii huyo wa vichekesho aliyeliza
wengi mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla, huku umati wa watu ukifunga katika
mtaa mzima nyumbani kwa Sharomillionea.
Pamoja na
vifo vya wasanii hao, kazi zao, uwezo wao utaendelea kukumbukwa na wengi, huku
kazi iliyobakia ni kuwaombea kwa Mungu ili wakapumzike kwa amani.
HERI YA MWAKA MPYA 2013! MUNGU IBARIKI KAZI YA WASANII, MUNGU WAREHEMU WALIOTUTOKA, MUNGU IBARIKI TAIFA LETU!!!
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :