TENGA AWASHUKURU WAJUMBE KWA KUPISHA WARAKA
Posted in
No comments
Monday, December 17, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
TENGA
AWASHUKURU WALIOPIGIA KURA WARAKA
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe
wa Mkutano Mkuu kwa kupigia kura waraka wa marekebisho ya Katiba, kwani
wametimiza wajibu wao.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema marekebisho ya Katiba
ni jambo muhimu, lakini lazima yapate ridhaa ya wanaohusika ambao ni
wajumbe.
“Nawasukuru
wajumbe kwa kupitisha jambo hili. Nawashukuru wote, waliokubali na waliokataa.
Ndivyo demokrasia ilivyo. Tulitaka waseme ndiyo au hapana, hivyo tulitarajia
kupata majibu yoyote kati ya hayo mawili.
Marekebisho
mengine yalikuwa ni maelekezo (directives) kutoka FIFA na CAF. Katiba yetu
inasema tutatekeleza maagizo ya CAF na FIFA, lakini kwa misingi ya utawala bora
tuliona ni lazima tupate ridhaa kutoka kwa wajumbe,” amesema.
Jumla ya
wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 waliunga mkono
wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa,
hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho
kikatiba.
Vipengele
vilivyoingizwa katika marekebisho hayo ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF
kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na
kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Vilevile
Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni
za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya
TFF.
Mkutano Mkuu
wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24
mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya
Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
RAMBIRAMBI
MSIBA WA AMINA SINGO
Shrikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha
aliyekuwa mtangazaji wa habari za michezo katika kituo cha redio cha 100.5 Times
FM, Amina Singo kilichotokea usiku wa kuamkia jana.
Msiba huo ni
mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya kazi na TFF, hivyo
mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.
Tutamkumbuka
kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla.
TFF tunatoa pole kwa familia za marehemu Amina Singo, ndugu, jamaa na
marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo mzito.
Mungu aiweke
roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi. Amina
SITA ZATINGA
ROBO FAINALI UHAI CUP
Timu sita
zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Uhai
inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20) wa klabu za Ligi
Kuu ya Tanzania.
Hatua ya robo
fainali ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es
Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitai maji Uhai
itafanyika Desemba 19 mwaka huu kwenye viwanja hivyo hivyo.
Timu
zilizofuzu kutoka kundi A ni Coastal Union ya Tanga, Mtibwa Sugar
ya Morogoro na JKT Ruvu ya Dar es Salaam. Kundi C ni Oljoro JKT ya Arusha na
Ruvu Shooting ya Pwani wakati iliyofuzu kutoka kundi A hadi sasa ni Azam
pekee.
Katika mechi
zilizochezwa leo asubuhi (Desemba 17 mwaka huu) Coastal Union na Mtibwa Sugar
zimetoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, wakati Uwanja wa Azam
ulishuhudia African Lyon ikiifunga Mgambo Shooting mabao 2-1.
Nafasi mbili
za robo fainali zilizobaki kutoka kundi B zinawaniwa na timu za Simba, African
Lyon na Polisi Morogoro. Mechi itakayochezwa leo saa 10 jioni katika Uwanja wa
Chamazi kati ya Polisi Morogoro na Simba ndiyo itakayoamua timu zitakazoungana
na Azam kutoka kundi hilo.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :