MKUTANO WA CHADEMA MKOANI KILIMANJARO NI M4C TUPU!
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imewataka wananchi kusimamia
Rasilimali zao kwa Kuwa ni wao ndio waathirika wakuu wa uharibifu na ufujaji wa
Rasilimali unaofanyika sasa hivi.
Akizungumza na maelfu
ya wananchi wafuasi wa chama hicho waliojitokeza kwa wingi katika
mikutano hiyo, Katibu Mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Dkt.
Wilbroad Slaa alisema kuwa ncwaandamizi wa chama hicho, itaka serikali kutoa
ufafanuzi kwa wani hii inarasilimali nyingi, ukianza na mlima
Kilimanjaro, mbuga za wanyama na madini ambayo kwabahati mbaya nchii imeshindwa
kuzithamini kwa manufaa ya wananchi.
“Wananchi wa nchi hii, imefika muda ambao, tunatakiwa kutambua kuwa rasilimali
zetu zinatakiwa zilindwe na Watanzania wenyewe, nchi hii ina madini mengi tu,
tuna bahati ya kuwa na Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, madini ya uraniam,
na vivutio vingi lakini kwa bahati mbaya rasilimali hizo tumeshindwa kuzifaidi
na badala yake tumebaki kuwa masikini,” alisema.
Alisema kuwa endapo wananchi hawatazinduka na kupigania haki zao, swala la
kuondokana na umasikini na uozo wa ufisadi ulitapakaa kila kona ya taifa hili
haitafika mwisho zaidi ya kuendelea kutafuna mifuoa yetu hadi kaburini.
“Tunawashauri wananchi kujitambua na kupigana kwa pamoja kulinda rasilimali za
nchi pamoja na kusukuma mbele lengo letu la kuleta ukombozi wa kifikra,
ukombozi wa kimaendelea na ukombozi katika siasa ya nchi hii,” alisema dkt.Slaa
alisema kuwa katika moja ya maazimio ya CHADEMA kwa mwaka huu, wamelenga kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu badhi ya maswala ambayo wao Kama CHADEMA wanafahamu ukweli huku serikali ikiendelea kuwafumba wananchi
Kiongozi huyo pia alikemea tabia ya baadhi ya maofisa katika jeshi l apolisi kutumika katika siasa ambapo alisema kuwa serikali inachangia kwa kiasi kikubwa kuchafua Jeshi la polisi kwa kuwatumia kama mashushu katika mikutano ya CHADEMA.
“Vijana wa wenzagu, ukombozi sio lele mama, ukombozi na mabadiliko kiuchumi, kimaendeleo, mabadiliko ya elimu, mabadiliko na ukombozi yanahitaji ujasiri na uthubutu wa moyo kufanya maamuzi magumu,” alisema
Kuhusu swala la Gesi ya Mtwara, Heche alisema, utafiti unaonesha kuwa Gesi iliyopatikana Mtwara, ambao unaujazo wa Trilioni 35 na kuifanya Tanzania kuwa ya pili kwa uzalishaji duniani, inaweza kuwalisha Watanzania kwa zaidi ya miaka 200 bila kufanya kazi yoyote.
Alisema kuwa maandamano ya wananchi wa Mtwara ni matokeo ya serikali kuendesha mambo yake bila kuwashirikisha wananchi wake, hivyo kuitaka serikali iangalie namna ya kukaa meza moja na watu wa Mtwara na kuwaeleza watanufaika vipi kutokana na Gesi hiyo baada ya Gesi
kupelekwa Dar es salaam.
Dkt.Slaa akiwasili mkoani kilimanjaro jana |
Mbunge wa Arusha Mjini-Godbless Lema akifanya yake |
Lema |
Ni Mwendo wa M4C sasa |
Aidha, Jafari alisema, ile dhana kuwa CHADEMA ni chama cha maandamano ni upotoshaji mkubwa na kuongeza kuwa maandamano ni haki ya mwananchi yeyote Yule anayejitambua na kuitaka serikali kujikita katika kutatua kero za wananchi wake na sio kutoa matamko yasiyo na msingi wowote.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :