JIDE AMEFANIKIWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Posted in
No comments
Sunday, January 13, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
MSANII wa muziki wa
kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jay Dee, jana
alifanikiwa kukamilisha ziara yake ya siku sita ya kupanda mlima Kilimanjaro,
ikiwa na lengo la kutangaza mlima huo na kujionea upekee wa kivutio hicho.
Katika ziara hiyo
iliyodhaminiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini (TANAPA), msanii huyo aliyeambatana
na mumewe ambaye ndiye anesimamia kazi zake, Gadna Habash, waliwasili kwenye lango kuu la
Marangu saa 12 jioni na kupokelewa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro
(KINAPA), Erastus Lufungulo.
Wawili hao walianza
safari ya kupanda mlima Kilimanjaro Januari saba na kufanikiwa kufika katika kilele
chake chenye urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.
Akizungumza kwenye
mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kushuka mlimani, Jay Dee, alisema
ziara hiyo imetoa mafunzo makubwa kwao na wakatoa wito kwa wasanii, waandishi
wa habari na watangazaji nchini, kutembelea vivutio hivyo ili kufahamu yale
wanayozungumza kuhusu hifadhi hizo.
“ziara hii imenipa
mwanga kama msanii, nimejifunza mengi na niwakumbushe tu wasanii wenzangu
kuchukulia zoezi la kupanda la kupanda mlima Kilimanjaro kama moja ya majukumu
na wajibu wao kama wananchi wa taifa hili,” alisema Jide
Kwa upande wake
mhifadhi wa KINAPA Lufungulo ametoa rai kwa wadau wote hasa wananchi wa kawaida
kushiriki kupanda mlima huo, kwa lengo la kukuza utalii wa ndani.
Mwisho.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :