BABA LEVO SINA BIFU NA LINEX

Posted in
No comments
Friday, February 15, 2013 By danielmjema.blogspot.com






MSANII anayefanya muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Baba Levo ameibuka na kuzungumzia uhusiano ulioko kati yake na msanii mwenzio katika kundi la Kigoma All Stars, Sunday Mjeda maarufu Linex.
 
 Baba Levo ambaye alikuwepo mjini hapa jana na kundi la Kigoma All Stars, alisema kuwa uzushi unaonezwa mtaani kuwa yeye na Linex haviivi ni uongo na kuongeza kuwa Linex ni ndugu yake na kamwe hawatakaa wagombane.

Baba Levo alisema kuwa kumekuwa na watu wasiokuwa na kazi wanaoeneza uzuzshi kwamba yeye na Linex hivi sasa hawazungumzi na kuongeza kuiwa kilichotokea kati yake na Linex ni tatizo dogo na sio kubwa kama inavyoelezwa.

“Kilichotokea kati yangu na Linex lilikuwa ni tatizo dogo sana, kuna Msanii ambaye ni mdogo wetu kutoka Kigoma, ambaye alimfuata Linex ili Linex amsaidie sasa baada ya yey kugoma kumsaidia dogo nilimfuata kumshauri lakini mwenzangu “alimaindi”

“Tulikaa na kuyazungumza na hivi sasa tunafanya kazi pamoja na wala sidhani kama kuna ugomvi wowote kati yetu, Linex ni mdogo wangu, Linex ni mwanangu tofauti na watu wanavyotufikiria, hatuwezi kugombana hata siku moja, lile tatizo limekwisha,” alisema.


Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .