MSECHU: “LEKA DU TIGITE SIO KUNDI”
Posted in
No comments
Friday, February 15, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
MSANII Peter Msechu amesema kuwa kundi la Leka du
tigite, maarufu Kigoma All Stars haiishi kwenye kucheza tu kama watu
wanavyodhani, Leka du tigite ni kampuni na haitakaa ivunjike.
Msechu alitoa maneno hayo jana katika Akizungumza katika hoteli ya Ossy Grand Hoteil ilikofikia kundi hilo jana tayari
kwa shoo ya Valentine kwa wakazi wa Moshi.
Alisema kuna watu wanaochukulia kundi lao kuwa ni
kundi la kuimba na kucheza tu bila kufahamu kuwa Leka du tigite ni kampuni
iliyosajiliwa kufanya kazi za kijamii kama makampuni mengine.
Alisema kuwa lengo la kuanzisha kundi la leka du
tigite lilikuja baada ya kuona Mkoa wa Kigoma ukiwa nyuma kimaendeleo wakati
kunawatu wenye uwezo kama akina Zito Kabweambao wanaweza kutumika kuiletea
kigoma maendeleo inayotakiwa na kuwakomboa wananchi wa mkoa huo kutokana na
umaskini.
Alisema kuwa baada ya kuanza wao kama wasani kuimba
nyimbo zao kukusanya fedha, ndipo wazo la kuunganisha wazawa wa kigoma lilipo
kuja na wala sio kwamba lengo lao ni kuimba tu basi.
Msechu alisema kuwa kundi hilo maarufu kama Kigoma
All Stars linaundwa na watu maarufu wenye nia njema na mkoa wa Kigoma pamoja na
maneo mengine ya Tanzania na kuongeza kuwa wanatarajia kufanya mambo
makubwa tu kwa wananchi zaidi ya kuimba.
Akizungumzia kimya chake Peter Msechu alisem akuwa
hivi karibuni amejipanga kutoa wimbo utakaokwenda kwa jina la Kumbe ambao
atamshirikisha Joh Makini na kuongeza kuwa amekuwa ni mtu wa kusafiri mara
baada ya kumaliza Tusker Project Fame ndio amekuwa kimya.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :