Njia zitakazotumika Kilimanjaro Marathon zatangazwa
Posted in
No comments
Sunday, February 10, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
PRESS
RELEASE
10/2/2013
Waandaaji wa Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kwamba mbio za
mwaka huu zitafanyika katika njia zile zile zilizotumika mwaka jana. Mbio hizo
limepangwa kufanyika tarehe 3 Machi 2013 mjini Moshi.
John Addison, Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, ambao ni waandaaji
wa tukio hilo alisema katika taarifa jana kwamba njia zitakazotumika kwa ajili
ya Kilimanjaro Marathon 2013 ni kuanzia Uwanja wa chuo cha Ushirika (MUCCoBS) kuelekea
katikati ya mji, na kisha kufuata barabara kuu ya kwenda Dar -Es- Salaam kwa
takriban kilomita 8 hadi 9, baadae watageuka na kurudi Moshi mjini kupitia katikati
ya mji, na badae watapandisha mwinuko kidogo kuelekea Mweka, "wanariadha watafurahia zaidi sehemu hii
kwasababu ina mandhari ya kuvutia na kutakuwa na washangiliaji wengi kando ya barabara”.
Addison anasema “sehemu ya kupandisha kuelekea Mweka inahitaji
kupanda kwa taratibu lakini kwa sababu Mlima Kilimanjaro ni kivutio na uwepo wa
wananchi wanaoshangilia muda unaenda haraka na kuwasaidia wakimbiaji kumaliza
mapema. Alisema kuwa kituo cha cha Mweka ambapo wanaridha wanageukia kurudi
uwanja wa Ushirika inakuwa ni takribani kilometa 32 tangu kuanza mbio ndefu ya
kilomita 42. Baada ya hapo kipande kilichobaki inakuwa ni mteremko kuelekea
uwanjani mwisho wa mbio na njia nzima ni mteremko tu.
Aliongeza kuwa kwa wale watakaoshiriki nusu Marathon, mbio
zitaanzia uwanja wa MUCCoBS ambapo pako tambarare na baadae watapandisha kwenye
mwinuko kidogo kuelekea Mweka kama ilivyo zile mbio ndefu kabla ya kurudi
umbali wa takriban km 10, kuelekea tena uwanjani.
Kutakuwa na meza za maji kama ilivyo kawaida na magari maalum ya
kunyunyizia maji mithili ya mvua kando ya barabara huduma ambazo zimeandaliwa
maalum kuwafanya wanariadha waendelee kuwa na nguvu wakati wote wa mbio hizo.
Kuhusu burudani, Addison alisema kuwa hali ya uwanjani itakua ya
kusisimua kutokana na burudani kali kutoka bendi za muziki wa nyumbani zitakazokuwepo,
chakula cha kutosha, nyama choma na vinywaji na bila kusahau mbio za kujifurahisha
za Vodacom 5km Fun Run ambazo pia zinatarajiwa kuleta msisimko wa aina yake.
“Ili kuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara zitakuwa
zimefungwa, asubuhi siku ya mbio, lakini kutakuwepo na njia mbadala kuzunguka
mji kwa ajili ya wakazi wa Moshi. Wakazi wa moshi ambao wanatarajia kukimbia
pamoja na wakimbiaji wengine watakaofika Moshi mapema wanaweza kuanza mazoezi
katika njia hizo hili kupata uzoefu wa njia na kujiandaa vizuri kwa ajili ya
mbio.
Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na
Kilimanjaro PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo ni pamoja na
Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon Walemavu), Tanga Cement,
CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha
Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya
Watu (UNFPA).
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :