GAMA AHIMIZA UFUGAJI WA NYUKI KILIMANJARO
Posted in
No comments
Friday, February 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, KILIMANJARO
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amewaagiza
wataalamu wa ufugaji wa Nyuki katika Halmashauri za mkoa, kuhakikisha wanaenda
vijijini kutoa elimukwa wananchi juu ya ufugaji bora wa Nyuki.
Gama ametoa agizo hilo baada ya kukabidhi mizinga
150 ya Nyuki na pikipiki 10 iliyotolewa na shirika la UNDP kwa kushirikiana na
serikali ya Jamhuri ya Tanzania.
Amesema ufugaji wa nyuki unahitaji uwepo wa
mazingira mazuri yatakayoruhusu kuwepo kwa miti ya kutosha ambayo nyuki
watatumia maua yake kuzalisha asali na kuwataka wanchi kuendelea kuhimizwa
kutekeleza amri ya kutokata miti ikiwa
ni pmoja na kusisitizwa kupanda miti kwa wingi.
Aidha Gama amelishukuru shirika la UNDP kupitia kwa
mwakilishi wake mkoani hapa, ndugu Francis Mkanda kwa juhudi wanazofanya
kuboresha maisha ya wana Kilimanjaro kupitia kilimo na ufugaji.
Hata hivyo
Mkuu huyo wa Mkoa, amesema Ufugaji wa ni Nyuki fursa ya ajira binafsi kwa mtu yeyote Yule,
kaya au kikundi na kuongeza kuwa kwa kutambua hilo, serikali ilishaanza kuzuia
ukataji, upasuaji na usafirishaji wa mbao kuanzia Februari 29 mwaka jana.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :