watu wafariki katika matukio mawili tofauti kilimanjaro
Posted in
No comments
Friday, February 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
WATU wawili wamefariki dunia katika
matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro likiwemo tukio la mtu kujinyonga kwa
kutumia kipande cha kanga na lingine la ajali.
Katika tukio la kwanza mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la Aloyce Msabaha (58), mkazi wa Kibosho Kitandu, Moshi Vijijini
alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kipande cha kanga na kuacha ujumbe mzito
kuhusiana na kifo chake.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo, Msabaha ambaye ni baba wa familia ya mke na watoto haifahamiki ilikuwaje
mpaka akafikia hatua ya kusitisha uhai wake japo taarifa ambazo
hazijathibitishwa zinadai ni wivu wa mapenzi.
“Usiku majira ya saa sita na nusu kuelekea
saa saba, tulisikia mbwa wakibweka sana, lakini hatukushtuka kutokana na
kulifahamu sana mtaa wetu kwa matukio ya Wanga, asubuhi tulivyoamka tukasikia
mayowe yakitokea upande wa nyumba ya mzee wetu, Msabaha, mimi nilikuwa wa
kwanza kufika kutokana na ukaribu wangu na familia yake, kumbe yale makelele ya
mbwa waliokuwa wanabweka usiku ni kwa ajili ya tukio hili,
“Tulikuta mwili wake ukiwa umening’inia
katika mti wa mwembe uani, nyumbani kwake, tuliushusha mwili na kukuta ujumbe
huu,” amesema mtoa habari huyo ambaye amekataa kata kata jina lake kutumika mtandaoni.
ACP-ROBERT BOAZ |
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro, ACP-Robert Boaz amesema, baada
ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema, polisi walifika katika eneo la tukio na
kukuta mwili wa marehemu pamoja na karatasi kilichokuwa na ujumbe.
“Marehemu alikutwa akiwa amejinyonga
kwa kutumia kipande cha kanga, alikutwa na kipande cha karatasi kilichokuwa na
ujumbe kwamba familia yake, mkena watoto wasisumbuliwe kwa chochote kile,
walindwe hata hivyo hatukuweza kufahamu chanzo cha kifo hicho,” alisema Boaz.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa
saba usiku ambapo inadaiwa kuwa mwili wa marehemu uligundulika asubuhi ukiwa
umening’inia katika mti wa mwembe jirani na nyumba ya marehemu.
Katika tukio la pili, Mtu mmoja mtembea
kwa miguu, Raphael Maro (48), mkazi wa Uru Kariwa aligongwa na pikipiki,
lililokuwa likiendeshwa na mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja
kutokana na kukimbia baada ya kusababisha ajali hiyo.
Kamanda Boaz amesema tukio hilo
lilitokea, Februari 5, majira ya saa 4 usiku, katika barabara ya Uru eneo la
makelele na kuongeza kuwa Jeshi lake linamsaka mtu huyo kutokana na kutoroka
baada ya kusababisha kifo cha mwenda kwa miguu ambaye alikufa papohapo.
Wakati huo huo Jeshi la polisi
mkoani hapa linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kukutwa na pikipiki 3 za wizi
katika eneo la Kahe, Wilaya ya Moshi Vijijini.
Taarifa kutoka kwa Kamanda wa polisi
mkoani hapa, zinasema kuwa mtu huyo, Stewart Elias (32), alikamatwa na pikipiki
hizo baada ya maaskari wa doria kugundua kuwa pikipiki alililokuwa anaendesha
halina namba za usajili.
Kamanda Boaz amezitaja pikipiki
zilizokamatwa kuwa ni moja aina ya Kinfan yenye cheses namba, LWAPCJL220A805284
injin namba KF157FM120A09290 pamoja na Lingken mbili, la kwanza lenye cheses
namba, chases namba LZK1502133956484 injin namba LK157FM111075648.
Boaz amelitaja pikiki la tatu aina
ya Lingken kuwa ni pikipiki yenye chases namba LZLK1502373A72319 injin namba
LK156FM1070172324 na kuongeza kuwa mpaka
sasa idadi ya pikipiki zilizokamtwa katika kipindi cha siku mbili zimefika
saba.
Kamanda Boaz alitoa wito kwa
wananchi ambao wamepotelewa na pikpiki zao kufika katika kituo cha polisi kutambua
pamoja na kuchukua pikipiki zao.
“Tunawaomba wananchi ambao
wamepotelewa na pikipiki kufika hapa kituoni kutambua mali zao na kuzichukua
kwa sababu hatuna sehemu pa kuzihifadhia,” amesema Boaz.
MWISHO.
Click here to Reply or Forward
|
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :