African Barrick Gold kutenga dola milioni 10 kila mwaka kwa ajili ya uwekezaji wa mfuko wa maendeleo wa ABG kwa mwaka 2013.
Posted in
No comments
Tuesday, March 19, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Afisa
Mtendaji Mkuu wa ABG Greg Hawkins akizungumzia Mfuko wa Maendeleo wa
ABG amesema mpaka sasa mfuko huo umewekeza dola za Marekani milioni 2.2
(zaidi ya shilingi bilioni 3.6) kusaidia kuboresha afya ya umma kwenye
jamii zinazo zunguka migodi yake.
Amesema
kwa upande wa elimu, Mfuko umetumia zaidi ya dola za Marekani milioni
1.9 (takriban shilingi bilioni 3) kuwekeza kwenye sekta muhimu na kuwa
uwekezaji wa mfuko huo umesaidia kujenga shule mpya na kuongeza idadi ya
madarasa kwenye shule nyingine ili kuwapa watoto wengi zaidi fursa ya
kupata elimu bora.
Vice
President Corporate Affairs Deo Mwanyika (kulia) amesema lengo kubwa la
kuwepo kwa mfuko huo ni kutaka kuhakikisha jamii iliyozunguka migodi
hiyo inafaidika na kuwa lmtazamo bado uko katika masuala muhimu kama
elimu, masuala ya maji, masuala ya afya na kwa kiasi Fulani masuala ya
miundo mbinu.
Akizungumzia
mgodi wa North Mara uliopo wilaya ya Tarime, amesema Mfuko umewekeza
dola za Marekani 800,000 (sawa na shilingi bilioni 1.3) kwa ajili ya
kuchimba visima vya maji ili kuwasaidia wananchi wapate maji safi na
salama ya kunywa.
Corporate
Manager – community Relations Steve Kisakye (wa pili kulia) akifafanua
jinsi Mfuko huo unavyoweza kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali,
ambapo ili kuboresha maisha ya jamii zinazozunguka migodi hiyo minne,
Mfuko wa Maendeleo wa ABG umeweka dola za Marekani milioni 1.4 (zaidi ya
shilingi bilioni 2) kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.
Mfuko
wa Maendeleo wa African Barrick Golg ulioanzishwa mnamo Septemba 2011
umeweza kusimamia uwekezaji wa kampuni ya ABG kwenye jamii katika
kipindi cha miezi 18 iliyopita na kufanikiwa kutekeleza zaidi ya miradi
50 yenye thamani ya dola za marekani milioni 7.5 (takriban shilingi
bilioni 12) katika kipindi cha mwaka 2011/2012.
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Afisa Mtendaji Mkuu wa
ABG Greg Hawkins amesema wanafurahi kuona mafanikio makubwa ambayo Mfuko
wa maendeleo wa ABG umeyapata kwenye kipindi cha miezi 18 mpaka sasa.
Ameongeza
kuwa walianzisha Mfuko huo kama sehemu ya jitihada zao za kuchangia
kwenye maendeleo endelevu nchini Tanzania na tayari mafanikio makubwa
yameonekana kwenye zaidi ya miradi 50.
Mfuko
wa Maendeleo wa AGB unashirikiana na jamii husika kubaishinisha vipau
mbele vyao ili wanajamii wenyewe wawe mstari wa mbele kwenye utekelezaji
wa miradi.
Kampuni
ya ABG inalipa gharama zote za uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo wa ABG
ili kuhakikisha kuwa asilimia kuwa asilimia 100 ya fedha za Mfuko huo
zinaenda moja kwa moja kwenye miradi ya jamii.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :