Wasanii wa Injili kushiriki tamasha la Tumaini Jipya Machi 31 mkoani Morogoro, Martha Mwaipaja, Stara Thomas, Masanja Mkandamizaji Ndani!

Posted in
No comments
Thursday, March 21, 2013 By danielmjema.blogspot.com

KAMPUNI ya QS Entertainment, imeandaa tamasha kubwa la ‘Tumaini Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Morogoro likihusisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.
Mkurugenzi-Mhonda
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph Mhonda alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji  maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani Morogoro likiwa na lengo kubwa la kueneza neno la bwana na mambo mengine ya kijamii katika kila mkoa watakapokuwapo.
Martha Mwaipaja akizungumza jambo na mwimbaji mwingine wa muziki wa Injili, Stara Thomas, aliyewahi kuwika pia kwenye muziki wa Kidunia, maarufu kama Bongo Fleva. 

=
 
 Martha Mwaipaja, akizungumza jambo.

 Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Joseph Mhonda, ambao ndio waandaaji wa tamasha akiwa mbele ya kamera ya Handeni Kwetu Blog.

Mkurugenzi wa QS Entertainment, Joseph Mhonda, akizungumza katika utambulisho wa Tamasha la Tumaini Jipya.

Mhonda, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa tamasha lao la ‘Tumaini Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Morogoro, linagusa hisia za wengi kwa kushirikisha wakali mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mhonda alisema kuwa alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji  maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani Morogoro.

 Martha Mwaipaja
“Tamasha hili limeanzia Morogoeo lakini litaendelea kwenye m ikoa mingine ya Tanzania  likiwa na lengo la kutoa tumaini kwa jamii,  na mapato yatakayopatikana yatasaidia  watu walio katika mazingira magumu” alisema Mhonda

Alisema katika tamasha hilo ambalo ni la aina yake kufanyika Tanzania, litapambwa na waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki ambao ni Bahati Bukuku, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki, Stara Thomas, Matha Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven.


Stara Thomas akiteta jambo na Martha Mwaipaja
 
Mbali na waimbaji hao  pia kutakuwa na kwaya mbalimali Rafiki Gospel Singers, Haleluya Kwaya, Victoria Kwaya na MTC .
Mhonda alisema sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia waimbaji hao pia watakuwa na muda maalum wa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa watu wote, pamoja na mbinu za kufaulu mtihani kwa wanafunzi.
Kwa mujibu wa waandaaji hao, Tamasha la Tumaini Jipya, ni fursa pekee kwa wakazi wa Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika kusherehekea siku Kuu ya Pasaka.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .