TFF YAONDOA ‘FREE PASS’ VIWANJANI
Posted in
No comments
Friday, March 15, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeondoa
utaratibu wa wadau wake kuingia bure kwenye mechi kwa kutumia tiketi maalum
(free pass).
Kutokana na uamuzi huo hakutakuwa
tena na pasi za bure kwa ajili ya kushuhudia mechi zilizo chini ya usimamizi wa
moja kwa moja wa TFF katika viwanja mbalimbali nchini.
Uamuzi huo umetokana na ukweli kuwa
free pass zimekuwa zikipunguza au kuchukua mgawo wote wa TFF kwenye mechi, na
wakati mwingine Shirikisho hulazimika kutoa fedha za ziada kugharamia pasi
hizo.
Pasi zote ambazo imekuwa ikitoa kwa
wadau wake hukatwa katika mgawo wa TFF katika mechi husika. Shirikisho hivi
sasa linapata asilimia nne tu ya mapato katika mechi za Ligi Kuu, ligi ambayo
hivi sasa inaendeshwa na Kamati yake ya Ligi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :