CCM YAKABIDHI MSAADA WA MIPIRA NA JEZI KWA BINGWA WA MKOA WA KILIMANJARO TIMU YA MACHAVA FC LEO
Posted in
No comments
Sunday, May 12, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
xxxxx
Mwandishi Wetu, Moshi
KATIKA kuelekea mchezo wa jana dhidi ya Flamingo FC ya
Arusha, Machava FC ambo ndio mabingwa wa ligi daraja la Tatu, mkoa wa Kilimanjaro,
wamekabidhiwa vifaa vya michezo na uongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya
Moshi.
Machava FC walikabidhiwa vifaa hivyo ambavyo ni
mipira mitano na Jezi, kama sehemu ya mchango wa Chama hicho kwa timu hiyo
ambayo kwa sasa ndio inayobeba Roho ya mkoa wa Kilimanjaro katika medani ya
soka.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifa hivyo
vilivyotolewa kwa timu hiyo na Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM, Jerry Silaa,
Katibu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini Aluu Segamba aliwahakikishia wapenzi wa
soka mkoani hapa kuwa wako tayari kushirikiana nao hadi mwisho wa Safari.
“Leo tunatimiza ahadi yetu kwa wawakilishi wetu, mabingwa
wa Mkoa timu ya Machava, tunaamini kuwa timu hii kama roho ya kilimanjaro
katika mchezo wa soka itafanya makubwa na kinachotakiwa ni kuwapa sapoti
inayostahili,” alisema Segamba.
Naye Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Abuu Masoud, baada
ya kupokea msaada huo kutoka CCM, alisema kutokana ushirikiano unaoneshwa na
wadau wa soka kwa timu yao wanaahidi kufanya vizuri katika michezo yao yote na
kuwapa raha wapenzi na mashabiki wa Machava mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande kocha msaidizi wa machava aliwaondoa hofu
mashabiki wa timu yake kuhusu hali ya Afya ya mshambuliaji wa kutumainiwa wa
klabu hiyo, Isa Kipese na kuelekea mchezo wa jana na kuongeza kuwa
kinachosubiriwa ni ripoti za madaktari wanaomshughulikia mchezaji huyo.
Machava FC ambayo inauwakilisha mkoa katika michezo
ya Mabingwa wa mikoa imekuwa ikipokea sapoti kutoka kwa wadau wa michezo mkoani
hapa ambapo hivi karibuni tu Mbunge wa Moshi Mjini, Filemon Ndesamburo na Mstahiki
Meya wa Moshi, Jafary Michael walitembelea kambi ya timu hiyo na kuchangia
fedha taslimu shilingi laki saba.
Katika hatu
nyingine chama cha Mapinduzi CCM pia imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa
timu ya Gillete Fc ya kata ya Kaloleni kama sehemu ya utekelezaji wa ilani ya
chama hicho za kutoa fursa nyingi za ajira kwa njia ya michezo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :