LUNDENGA NA MISS TANZANIA WAWAPA MAKAVU MISS KIBAHA 2013
Posted in
No comments
Sunday, May 12, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
HASHIM LUNDENGA |
Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Miss Tanzania ikiongozwa na
Mkurugenzi wa Kampuni ya International Agency ikiongozwa na Mkurugenzi
wake pia Mratibu Hashim Lundenga imewafunda ipasavyo warembo
wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Kibaha 2013 litakalofanyika
Mei 17 katika ukumbi wa Container mailimoja Kibaha.
Akizungumza wakati alipowatembelea
katika kambi yao warembo hao Lundenga aliwataka washiriki hao wajijengee
hali ya kujiamini na kila mshiriki asimwogepe mshiriki mwenzake huku
akiwataka kila mmoja awe amejiwekea lengo la kufika katika shindano la
Kanda na hatimaye taifa.
Aidha Lundenga amewaasa warembo hao
kumpa sapoti mrembo atakayetwaa taji hilo ,” endapo mrembo mwenzenu
yeyote ataiobuka na kutwaa taji lazima mumpe sapoti kubwa kwani ‘crown’
huvaliwa na mrembo mmoja tu hivyo nawatakia kila la kheri katika
shindano lenu na niwaahidi tutakuwa pamoja hadi siku ya shindano”alisema
Lundenga.
Mwisho Lundenda alimazia kwa kusema
kuwa mrembo atakayeonesha utovu wa nidhamu atatolewa katika shindano
hata kama itakuwa ni siku ya fainali hivyo amewataka wawe makini wakati
wote.
Wakati huohuo Miss Tanzania 2012
Brigite Alfred aliyeambatana na kamati hiyo alitumia fursa hiyo kutowa
mashaka ya mrembo kupangwa kuanzia katika ngazi ya awali hadi taifa.
“Warembo wenzangu kwanza nawapongeza
kwa hatua hii ya kujitosa kushiriki kwani ni hatua kubwa kwa sababu hata
mimi nilianzia katika ngazi ya awali kama hii lakini tangu nilipoingia
katika shindano hilo nilijiona ni mshindi hali iliyonijengea kujiamini
hata nilipokwenda katika shindano la Kanda na hatimaye taifa hivyo
nawatakia kila la kheri.
Shindano hilo linaloandaliwa na
Kampuni ya Linda Media Solution litapambwa na bendi ya Mashujaa huku
kiingilio kikiwa ni sh. 10,000 kwa VIP na siti za kawaida sh. 6,000.
Shindano
hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji
chake cha Redds Premium Cold, Shear Illusions, Fredito Entertainment,
CXC Africa, Multichoice DSTV, Times FM, Michuzi Media Group (MMG),
Santorine Holiday Resort ,PR.Promotion, Aco Catering Servises , Amazon
Night Club na Panandipanandi Pub
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :