Clouds wakunjua makucha yao dhidi ya Lady Jay Dee
Posted in
No comments
Wednesday, May 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UONGOZI wa Clouds Media Group kwa kupitia Mkurugenzi wao wa
Utafiti na Matukio, Ruge Mutahaba, umemtaka msanii wa Bongo Fleva, Judith
Wambura, Lady Jay Dee ajipange na kupokea changamoto badala ya kutafuta mahali
kwa kujiegemeza kwa kueneza matusi kwao.
Clouds Media jana walifungua mdomo kwa mara ya kwanza kwa
kipindi cha miezi mitano tangu Jay Dee alipokuwa akiwarushia makombora kwa
madai kuwa wameharibu soko la muziki wa Bongo Fleva sambamba na kuitangaza
bendi ya Skylight kwa ajili ya kuiangamiza Machozi Bendi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam ambapo pia alikuwa
akirushwa moja kwa moja katika redio ya Clouds FM, Mutahaba alisema Jay Dee
amekuwa akilalamikia mambo mawili ambayo ni bendi ya Skylight na matangazo yake
yaliyoshindwa kurushwa hewani japo alilipia Sh 240,000.
Alisema suala hilo walilimaliza baada ya kumueleza kuwa
redio yao haiwezi kukataa matangazo kwakuwa ndiyo wanayowafanya waendelee kuwa
kinara katika suala zima la kuiendesha Clouds FM.
“Nilimwambia kamwe hatuwezi kukataa matangazo na kama kuna
lolote limefanyika, basi ni kwa bahati mbaya, ukizingatia kuwa tayari
alishafanya kazi nyingi pamoja na kupewa urahisi kwenye kazi zake kwa kupitia
Clouds FM.
“Pamoja na yote hayo, bado matusi na kejeli yaliendelea hasa
katika mitandao ya kijamii jambo lililotufanya tuamuwe sasa kujibu japo hapo
kabla tuliamua kubaki kimya kwa ajili ya kulinda hadhi ya kazi zetu,” alisema.
Kuhusu shutuma za kuitangaza zaidi Skylight Bendi, Ruge
alisema bendi hiyo si mali ya Joseph Kusaga, Mkurugenzi wao wala yeye, kama
madai hayo yanavyotolewa bila kufanya utafiti, isipokuwa ni mali ya Sebastian
Ndege.
“Kama kuna mvutano kati ya Machozi Bendi na Skylight basi ni
wa kibiashara maana wote wanalipa fedha za matangazo na kama chanzo ni Jay Dee
kuporwa wanamuziki wake, hilo si jambo geni kwenye muziki.
“Dada yangu Asha Baraka asingekuwa makini angelia sana,
maana kila bendi inayoanzishwa au kuendeshwa lazima ichukuwe wanamuziki kutoka
kwake, ukizingatia kuwa ni jambo la kawaida hivyo tumuomba Jay Dee atumie
busara katika hili pamoja na kuumiza kichwa kupokea ushindani na changamoto
kama hizo za kuchukuliwa wanamuziki,” aliongeza Ruge.
Aidha, Ruge alisema Clouds FM ni redio ya watu binafsi,
hivyo si ina utaratibu wake katika utendaji wa kazi, ikiwapo kuchagua nyimbo au
kuacha kupiga kama kuna mtu amekwenda kinyume, hasa wale wanaopita nje na
kuanza kuwatusi, kuwakejeli bila kukumbuka fadhira walizofanyiwa kabla ya kuwa
maarufu wao.
Pia alisema Clouds FM ipo tayari kufanya majadiliano ya wazi
na mtu yoyote mwenye hisia tofauti juu yao, huku ikiwataka wasanii waongeze
bidii katika kazi zao ili wasimlaumu mtu wanapoanguka na kuwapisha wengine,
maana muziki unaonekana ni wa kupokezana vijiti.
Katika siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari hasa
hasa kwenye mitandao ya kijamii nchini kumekuwa na taarifa rasmi na zisizo
rasmi kutoka kwa Mwanamuziki Lady Jaydee alilalamikia Kituo chetu cha Clouds FM
na wakurugenzi wake Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.
xxxxx
SPEECH YAKE HII KAMA MNAITAKA PIA
RUGE MUTAHABA
Kwa mtazamo wangu, kila mwananchi ana haki ya kutoa maoni
yake ingawa kwenye nchi yetu ya Tanzania, tumezoea maoni hayo kutolewa kwa
lugha ya ustaraabu na staha.
Maoni kuhusu nani wa kuja kwenye msiba wako au nyimbo za
kupigwa kwenye msiba wako ni haki ya kila mwananchi na hakuna atayeuingilia
uamuzi huo. Maoni pia ya redio gani mtu anaipenda au tv gani pia nayo ni utashi
wa mtu mwenyewe.
Uongozi wa Clouds FM ulikuwa umefikia maamuzi ya kutojadili
jambo hili kutokana na kuamini kuwa ni tatizo binafsi la mtu na sio jambo lenye
maslahi ya Taifa hivyo kwa uhalali linahitaji majadiliano au mazungumzo
binafsi.
Sura ambayo jambo hili limewekwa na kulifanya kama dharura
ya kitaifa sio sahihi kabisa kutokana na
kukosekana na hoja za kina za kuhitaji majibu na pili kukosekana kwa ujumla wa tija
kwa tatizo hili kitaifa.
Bado ninaamini linatakiwa kubaki kama tatizo la mtu binafsi
ila inapofika taarifa zikapotoshwa kwa nia ya kuwapa mtazamo tofauti
wasikilizaji wetu, Clouds FM inataka kuweka maslahi ya wasikilizaji, wabia wetu
wa biashara na watanzania wote mbele kwa kuwapa taarifa sahihi za jambo hili.
Clouds Media Group inapata lawama kubwa sana kutoka kwa watu
wengi ambao pamoja na kuunga mkono ukimya wetu wanajiuliza ni kwanini
hatukufanya jitihada za kumaliza tatizo hili bila kufika hatua iliyofikia sasa
ya matusi, kebehi na vitisho kutwa vinavyoelekezwa kwetu na pia vinaendelea
kuichafua tasnia ya muziki hasa hasa Bongo flava; ambayo imefika mahali
inaonekana kila changamoto inayomkabili msanii wa Bongo flava lazima itatuliwe
kwa njia za mabavu (matusi, vitisho na kuchafuana).
Lawama hizo sio za
kweli na naomba nirudi nyuma kidogo kwenye historia ya jambo hili. Tarehe
14 mwezi wa 12 mwaka 2012 kwenye tweeter account ya Jaydee, alipost kifuatacho:
Nilichofanya ni kumpigia simu na kuzungumza nae. Akasema sijaandika kwenye blog chochote,
nikamwambia Jide mi nakuheshimu sana. Nimekupigia kwasababu naamini kama kuna
kitu chochote ni bora nisikie kwako, nategemea na wewe pia utanipigia iwapo
kuna jambo lolote lile. Tulikotoka sisi
hatutakiwi kuendeshwa na majungu na maneno ya mtaani.Hiyo ilikuwa tarehe 14
mwezi December mwaka jana. Baada ya kama dk 10 hivi akanitumia msg ( ambazo
bahati nzuri nilizihifadhi) na kusema ni kweli alikuwa ananizungumzia mimi kwa
sababu kuna vitu kadhaa vinamsumbua na aliambiwa mimi ndo nilihusika navyo.
La kwanza, ‘nililipa matangazo ya shs laki mbili na 40 ila
hayajachezwa na wala sijarudishiwa hela yangu, nimeambiwa umekataza matangazo
yangu ya Nyumbani lounge yasipigwe’.
La pili, naruhusu watangazaji wangu wamtukane ikiwa ni
pamoja na kupromote zaidi bendi ya Skylight.
Pamoja na kwamba yeye alinitumia message, mimi nilimpigia
simu na kumpa ufafanuzi wa yote hayo niliyosema hapo juu.
Nikasema, Biashara yetu sisi ni matangazo…..kwanini
tukataze matangazo yako yasipigwe?? Labda bahati mbaya tu, jamaa anayebook
matangazo alipitiwa kuyabook kibinadamu ila Gadna si anakuja hapa kila wakati,
kwann asimkumbushe tu?? Tutayasogeza tu mbele hadi wiki inayofuata, kwanini
niyakataze wakati muda sio mrefu tumetoka kuleta biashara ya Repa bora wa bendi
hapo hapo Nyumbani lounge.
Niliendelea kujibu kuwa sio kweli kabisa, siwezi kuruhusu jambo
kama hilo na kama ni kweli mtangazaji anamtukana anifahamishe ni nani na kwenye
kipindi gani, nitasikiliza kipindi na kama ni kweli nitamfukuza kazi ( Clouds
ina mitambo ya kuhifadhi matangazo yake yote kwa takribani miezi 9).
Hili nilimjibu kwa kirefu kidogo ikiwemo kumwambia akaze buti maana
Skylight Band wanakuja juu nk nk. (Skylight Band ni bendi inayofanya vizuri
sana hapa mjini na ilipoanza ilichukua baadhi ya majina makubwa kutoka Machozi
Band).
Baada ya kumaliza mazungumzo tuliagana vizuri tu kwa miadi
ya kukutana nikirudi maana nilikuwa safarini.
Kwahiyo ukiniuliza Jaydee anacholalamika ni nini??? Jibu
langu litakuwa ni hayo mambo mawili maana hata nyie watanzania wenzangu
mnaosoma mitandao ya kijamii mtakubaliana na mimi kuwa amekuwa anashambulia
personality zetu, mimi na Mkurugenzi mwenzangu bila kuweka wazi hoja za msingi
kuhusu yale anayotutuhumu nayo.
Nimejitahidi sana kuelewa tatizo lake hasa ni nini na imekuwa inanipa
shida kidogo?? Nimejitahidi sana kufikiria ni mirija ipi ya biashara kwake
imeingiliwa, nakosa majibu???
Clouds FM ni ya watu na watu wanaweza kufanya makosa kweli
na hata kusababisha matangazo ya laki 2 na 40 yasirushwe, kwa hilo
nilishazungumza na Jaydee na kuomba radhi toka tarehe 14 December 2012. Clouds
FM haina ubia wowote ule na Skylight Band (ni bendi iliyoanzishwa na Mtanzania)hivyo
kuipromote ni katika misingi ile ile ya biashara kama tunavyopromote bendi
yeyote ile na vilevile Clouds FM pia haihusiki kabisa na kutetereka kwa
biashara ya chakula, vinywaji na bendi inayofanyika Nyumbani lounge.
Inashangaza hata kuhusishwa na biashara ya Nyumbani lounge…!!!
Sina ugomvi binafsi na Jaydee wala Gadna, na tarehe 12
February mwaka huu, nilienda kuazima stools kwa ajili ya shooting kutoka kwenye
sehemu yao ya biashara ingawa yeye amekiri kuwa na ugomvi mkubwa na sisi
binafsi na Clouds kama chombo.
Nyimbo yake iliyotoka ya Joto Hasira ilipokelewa vizuri sana
kulinganisha na nyimbo mbili zilizopita ‘Yeye’ na ‘Mimi ni mimi’ ambazo
hazikufanya vizuri pamoja na jitihada kubwa ya kuzipromote. Joto Hasira iliacha
kupigwa kutokana na shinikizo lake mwenyewe, ikiwa imeshachezwa mara 48 ndani
ya wiki tatu toka imetoka wote tulipigwa na bumbuwazi na kujiuliza ni kitu gani
tumefanya kuambiwa hatupigi nyimbo na lawama nyingine. Kama ofisi tukaona tukae
kimya na kusubiri hatua inayofuata ukizingatia tuliendea kupiga nyimbo na video
hata baada ya maneno makali ya mwanzo. Kauli haikubadilika, mbaya zaidi kauli
za kebehi na kuchafuana zikaongezeka hadi kufikia uamuzi wa sisi kama taasisi kuamua
rasmi kutopiga nyimbo zake hadi atakapofuta kauli zake na kuomba msamaha.
Kupiga au kutopiga nyimbo kwa kituo cha redio ni jambo la
kawaida na kwasababu ni chombo binafsi ni muhimu kwa watu kama Jaydee na
wasanii wengine (na hata wananchi wa kawaida) kuelewa kuwa kila ofisi ina
taratibu zake na iwapo utatokea ukiukaji wa taratibu hizo, policy ndo
zinaongoza maamuzi. Hebu tujiulize,
mbona sio mjadala wa Taifa msanii Diamond hapigwi karibu miezi sita sasa kwenye
station ya Magic FM, Ray C na Ali Kiba kwa karibu mwaka mzima walikuwa nyimbo zao
na video hazipigwi na East Africa hadi walipoomba msamaha, hadi Yanga kwa muda
mrefu walikuwa hawatangazwi habari zao kwenye chombo kimoja cha habari. Hayo ni
mambo ya ofisi binafsi na hakuna anayeweza kulaumu maamuzi hayo.
‘Management reserves the right of admission’……nani hajaona
kibao hiki kwenye hoteli nyingi tu nchini, nani asiyefahamu kuwa kuna hoteli
ambazo ukienda kama mwanamke peke yako unakataliwa? Hizi ni taratibu na kila
mahali zipo…..hata nyumbani lounge ndo maana Sam Machozi ambaye yuko Skylight
Band zamani alikuwa mwanamuziki wa Machozi Band amepigwa marufuku pale Nyumbani
lounge na halalamiki maana ni sehemu binafsi na ina taratibu zake. Ni tofauti
na sehemu za wazi za umma kama Mnazi mmoja au kituo cha basi cha Magomeni.
Clouds Media Group inafuata taratibu zote za nchi na za
kimkoa ila na yenyewe pia inaweka taratibu zake za uendeshaji. Sasa isifike
mahali Clouds inapoweka taratibu zake hizo na kuzitekeleza inaonekana inafanya
makosa. Yaani hata tarehe za kufanya
show nchi hii tunatakiwa kupeleka maombi sehemu ili watu zaidi ya mmoja
wasifanye show kweli??? Kwanini
tunachanganya ushindani na fitina…..acha ziwepo bendi 10 zinazoshindana,
kuanzishwa kwa bendi nyingine kusiangaliwe kama fitna. Na hata mtu akianzisha bendi kwa kuchukua
wanamuziki kutoka kwenye bendi nyingine, si ndio dhana ya ushindani???
Kama ni kulalamika kuanzishwa kwa bendi nyingine au
kuchukuliwa wanamuziki, Dadaangu Asha Baraka si angeshafanya maandamano nchi
nzima. Ila wote tunatambua kuwa ni jasiri ndo maana anatulia na kuanza upya.
Mbona watu hawalalamiki
baa zinapofunguliwa 10 mtaa mmoja, au saloon za nywele, moja jirani na
nyingine. Ni lazima tukubali na tuzoea ushindani.
Pamoja na ushindani kingine ninachoomba kuwasihi watanzania wenzangu hasa hasa
wasanii wetu zaidi ni kuwa kila mtu na
kila kitu kina ‘shelf life’. Watu wa zamani naamini wanamkumbuka Power
Mabula….alikuwa anatisha sana wakati ule. Au nani anaweza kusahau umaarufu wa
Mzee Nobert Chenga na Kundi la Muungano cultural troupe au labda huko ni nyuma
sana; nani anamkumbuka Kanda Bongo Man, alicharge laki moja enzi hizooo….au
labda hapa katikati umaarufu wa Muumini, Mr Nice au mtu kama Saida Karoli
(alijaza Stadium). Wote hao walikuwa maarufu sana. Sasa wasanii hawa na wengine
wanaokuja wasipojiandaa kuelewa kuwa kila kitu kina muda wake, tutakuwa na
taifa la vijana ambao asubuhi mpaka jioni badala ya kuhangaikia fursa nyingi
zilizopo wataishia kutafuta mtu wa kumlaumu.
Ni lazima Edibily Lunyamila atarithiwa sehemu yake na kina
Mrisho Ngassa ambaye naye muda utapita ni lazima atawaachia kina Simon Msuva.
Wapo watu kama kina Dully Sykes walioanza kujiandaa kwa kuwaachia kina Diamond
na wao kufungua studio na kuwa maproducer. Suala la kupokezana vijiti
halikwepeki kuanzia makazini, mpirani na hata kwenye sanaa. Cha kufanya ni kujiandaa
kwa maisha yako baada ya kugawa kijiti chako.
Taarifa za kutaka kuua muziki wa Bongo flava kwa makusudi
zinashangaza, ili iweje sasa??? Clouds inategemea matangazo ya biashara kama
asilimia 95 ya mrija wa mapato na muziki tunaopiga redioni ni sehemu ya maudhui
kwahiyo hakuna namna yeyote ile tutataka muziki huo upotee. Tunafanya juhudi
zote hizi kwasababu tunahitaji nyimbo bora na wasanii bora ili tuweze kuendelea
kuwa kituo bora cha redio.
SUMMARY YA MSIMAMO WETU
Fursa:
Uganda endorsment
TZ ringtones
Album sales – Kina Mamu.
DVD live performance shows.
Meeting ya wasanii wote watoe maoni.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :