KIPANDE CHA NYAMA KIMEKUTWA NYUMBANI KWA SHEIKH SHARIFF KIKIWA KIMEANDIKWA JINA LA ALLAH - DAR-ES-SALAAM
Posted in
No comments
Wednesday, May 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Sheikh Sharifff Mikidadi akiwa ameshika nyama hiyo akimuonesha mwandishi wetu huko nyumbani kwake Magomeni jijini Dar-es-Salaam. |
Na Mwandishi wetu maalum.
Siku chache baada ya tukio la
kugundulika kwa nyama ya ng'ombe iliyoandikwa kwa maandishi ya lugha
ya kiarabu jina la Mwenyezimungu yaani ALLAH huko nyumbani kwao
Sheikh Shariff Mikidadi eneo la kata ya Kiloleni Tabora mjini, tukio
la aina hiyo limejitokeza tena huko nyumbani kwake eneo la Magomeni
jijini Dar-es-Salaam na kusababisha mshangao mkubwa kwa watu
walioshuhudia.
Kutokea kwa kipande hicho cha
nyama ambacho kilitokana na nyama ambayo ilikwenda kununuliwa kwenye
moja ya maduka ya nyama eneo la Magomeni kwa ajili ya kitoweo
nyumbani kwa Sheikh Shariff,,maswali mengi yameendelea kujitokeza
na kukosa majibu hata kufikia hatua kwa wengine kumwachia
Mungu.
Maelezo ya awali yaliyotolewa
na mmoja wa kaka wa Sheikh Shariff anayefahamika kwa jina la
Abdillah Mikidadi alithibitisha kuwa mara baada ya nyama hiyo
kufikishwa nyumbani kwa Sheikh Shariff taratibu za mapishi
ziliendelea na baada ya kuiva kipande kimoja kilionekana kikiwa
kimeandikwa maandishi hayo ya kiarabu kwa maana ya ALLAH.
Alisema watu mbalimbali
wakiwemo baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wamefika
nyumbani kwa Sheikh Shariff kushuhudia kipande cha nyama hiyo na
huku wengine wakizidi kukumbwa na mshangao.
MAELEZO YA SHEIKH SHARIFF MWENYEWE.
Alipohojiwa kuhusu kuwepo kwa
tukio hilo ambalo pia limejitokeza katika familia yake tena kwa
mara ya pili mfululizo,Sheikh Shariff Mikidadi ambaye pia ni
kijana mwenye historia kubwa kutokana na kuzaliwa kwake katika
mazingira ya miujiza,alisema kuwepo kwa nyama hiyo ni tukio
linalodhihirisha uwepo wa Mwenyezimungu na kwamba hakuna haja
ya kuleta fikra potofu juu ya hilo.
Sheikh Shariff aliendelea
kusema kuwa jambo la msingi kwa waumini wa dini ya kiislamu
ni kuimarisha imani zao kwa kufanya ibada ipasavyo na
kumtukuza Mola wao na si vinginevyo.
''Mimi binafsi katika hili
naamini kuwa ALLAH anadhihirisha uwepo wake kwetu sisi na kwamba
kuna haja kwa waislamu kushikamana katika dini yao na kwamwe
tusifarikiane na kusababisha madhara kwetu sisi kama waislamu
pia hata na kwa wenzetu wa dini nyingine na hata wale
wasiokuwa na dini''alisema Sheikh Shariff
Aidha katika siku za hivi
karibuni tukio la kugundulika kwa nyama ya aina hiyo
lilijitokeza nyumbani kwao Sheikh Shariff huko kata ya Kiloleni
Tabora mjini ambapo tukio hilo liliripotiwa katika vyombo
mbalimbali vya habari na kushangaza idadi kubwa ya watu.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :