SILAHA 26 ZA STARS KUIANGAMIZA MOROCCO HADHARANI
Posted in
No comments
Friday, May 17, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen jana (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26
watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya
Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.
Katika
kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi
kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya
kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.
Wapya
aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1
jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent
Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi.
Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.
Kikosi
kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho
kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya
kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa
ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na
Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam),
Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent
Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna
Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya
(Azam) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva
(Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na
Zahoro Pazi (JKT Ruvu).
Kocha
Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo
Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji
atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa
mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.
Awali
TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya
Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo,
wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo
lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.
Kwa
upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka
huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF
ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :