WANYWAJI WAPINGA VIROBA KUPIGWA MARUFUKU
Posted in
No comments
Wednesday, May 15, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Wajumbe wa Kamati
ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea
kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Dar es Salaam hivi karibuni.
************
Na Mwandishi Wetu.
BAADHI ya
wananchi jijini Dar es Salaam, wamelalamikia hoja iliyozuka bungeni wiki hii
kwamba kinywaji cha Konyagi aina ya Kiroba kipigwe marufuku
nchini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao, walisema endapo
serikali itachukua uamuzi wa kupiga marufuku kinywaji hicho, watarudia kunywa
pombe aina ya gongo ambayo ni hatari kwa afya zao.
Mkazi wa Mbagala,
Faustine Mwiruka aliyekutwa kwenye baa ya Kisuma, aliiasa Serikali kutothubutu
kukubali kinywaji hicho kupigwa marufuku, kwani ikifanya hivyo wengi wa wananchi
wenye kipato cha chini wataanza tena kunywa gongo na pombe za
kienyeji.
Itabidi tufanye kama Zambia ambao wamezuia viroba, lakini nchi
nzima imejaa viroba vya Malawi, Zaire na Burundi, lazima tuiadhibu serikali
ikose kodi kote kote, bia hatunywi, viroba vya nje tutakunywa, pamoja na
gongo.
Alisema haingii akilini kukihusisha kinywaji hicho na ajali za
magari, akidai kuwa hata kabla ya viroba kuingia sokoni ajali zilikuwepo
nyingi.
"Sisi tuna imani na viroba kwa vile vina ubora wa uhakika tofauti
na pombe ya gongo ambayo inapikwa bila kupimwa ubora hivyo ni hatari kwa usalama
wa afya zetu." alisema Mwiruka.
Naye Ali Hassan mkazi wa Kinondoni kwa
Manyanya, alisema, wanaotaka viroba vipigwe marufuku hawawatendei haki wananchi
wa kawaida ambao kwa asilimia kubwa hawana uwezo wa kununua bia ambazo bei yake
ni kubwa.
Mwandishi wetu aliyetembelea maeneo ya Ilala Kota Mchikichini
alifanikiwakuhojiana na wakazi wa eneo hilo ambao wengi wao walisema kuwa jambo
hilo lililozushwa wiki iliyopita wanaamini ni njama za wafanya biashara toka
nchi jirani ambao hawaitakii mema Tanzania kwa kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia
kunakuza pato la Taifa.
Juma Pingu alisema kuwa haoni sababu ya kupiga
marufuku viroba kwakuwa ni pombe ya wanyonge na kuwataka wabunge kuthamini
bidhaa za nyumbani kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni
mwa wiki hii, Mkurungenzi Mkuu wa Konyagi, David Mgwassa alisema kuwa kwa
kipindi kirefu kumekuwa na mchezo mchafu wa kuharibiana jina sokoni kwa kutumia
baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini, kampeni inayoendeshwa na makampuni
yenye uhusiano na makampuni makubwa ya pombe duniani yasiyo penda, nchi za
afrika zizalishe pombe zake, bali ziendeleee kununua kutoka Ireland, wales.
Kenya and uingereza.
Wadau hao wa Pombe nchini walifikia uamuzi wa kutoa
maoni hayo baada ya kuona kuwa kinywaji chao Kiroba kinapigwa vita lukuki kwenye
magazeti. Huwezi ukahusisha viroba na piki piki, kwani nchi hii ina piki piki
laki tatu, na wananchi million 43, uhusiano wake uko wapi, kwanza hata leseni
hamuwapi?
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :