MICROSOFT, UHURU ONE WAANZA MAJARIBIO YA TEHAMA
Posted in
No comments
Wednesday, May 15, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uhusiano wa Microsoft Africa, Louis Otieno,
Louis Onyango Otieno akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mihayo Wilmore na Mkurugenzi wa
Utambuzi COSTECH, Faith Shimba.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMPUNI za Microsoft na Uhuru One, wameanza mpango wa
majaribio wa utoaji wa elimu ya Teknolojia ya Mawasiliano (Tehama) kwa kutumia
mkongo wa Taifa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lengo likiwa kuibua
uvumbuzi mpya katika sekta hiyo.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Uhusiano wa Microsoft Africa, Louis Otieno
alisema mpango huo utachukua miezi sita hadi mwaka mmoja.
Alisema mpango huo umewalenga wanafunzi kwa kuwa ndio kundi kubwa ambalo
linaingia katika shughuli za uzalishaji ikiwa ni pamoja na ajira, ujasiriamali
na ukweli kuwa ngazi ya elimu ya juu ndipo ambapo wanafunzi wanakuwa katika
hali ya kuweza kubadilika.
"Tumeangalia ngazi ya vyuo kwa kuwa ndio ambapo wanafunzi wanabadilika
na hata kuweza kufanya uvumbuzi" alisema na kuongeza kuwa Tanzania ina
vipaji vngi ambavyo vimeweza kufanya uvumbuzi katika eneo jingine lakini sio
katika Teknohama.
Awali akizungumza katika mkutano huo, Mtendaji wa wadau wa Uhuru One,
Mihayo Wilmore alisema mpango huo umelenga watu kuweza kuutumia mkongo wa Taifa
katika shughuli za habari na mawasiliano hususan maeneo ya vijijini.
Alisema mkongo wa Taifa umefika hadi katika ngazi ya wilaya lakini lakini
umekuwa hautumiki hali ambayo alisema chini ya makubaliano hayo yana lengo la
kuhakikisha hali inakuwa tofauti na majaribio yanayofanyika ni endelevu na
wadau zaidi wanakaribishwa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :