KAMPENI ZAELEKEA UKINGONI ZIMBABWE

Posted in
No comments
Monday, July 29, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Kampeini za kisiasa nchini Zimbabwe zinamalizika hii leo kabla ya uchaguzi mkuu hapo Jumatano wiki hii. Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change ambaye pia ni Waziri MKuu ,Morgan Tsvangirai, hii leo atahutubia mkutano wa hadhara mjini Harare katika uwanja alikofanya mkutano wake hio jana Rais Robert Mugabe.

Viongozi hao wawili wamekua katika serikali ya muungano tangu mwaka wa 2008 na wametofautiana kuhusu muda uliowekwa kufanyika uchaguzi. Kumekua pia na madai ya wizi wa kura, na vitisho dhidi ya wafuasi wa MDC.

Shirika la kimataifa linalotathmini hali ya mizozo The International Crisis Group limeonya kwamba hakuna mazingira ya uchaguzi huru na haki Zimbabwe.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .