UCHAGUZI MKUU MALI WAPONGEZWA NA WENGI
Posted in
No comments
Monday, July 29, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Uchaguzi mkuu wa Urais nchini Mali umesifiwa kwa Namna ambavyo ulifanywa. Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema kuwa wapiga kura wengi walijitokeza kupiga kura wakati wachunguzi kutoka barani Ulaya wakisema kuwa uchaguzi wenyewe umefanyika bila vurugu.Hata hivyo idadi ya waliopiga kura katika eneo la Kaskazini ilikuwa chini ikilinganishwa na maeneo mengine ya nchi.
Wadadisi wanasema huenda kukawa na duuru ya pili ya uchaguzi huo.Wachunguzi wameelezea kuwa wapiga kura walijitokeza kwa wingi katika mji mkuu wa Bamako pamoja na maeneo mengine ya Kusini mwa taifa hilo.Mwandishi wa habari wa BBC nchini humo amesema kuwa wengi wa wapiga kura walitaka vidole vyao kutotiwa wino.
Amesema waasi wa Tuareg ambao wanadhibiti eneo kubwa la Kaskazini wamepinga uchaguzi huo licha ya kukubali shughuli hiyo kuendelea.Wagombea 27 walishiriki kwenye uchaguzi huo na ikiwa hapatakuwa na mshindi bayana huenda duru ya pili ikafanyika tarehe 11 mwezi Agosti.
Hata hivyo wachanganuzi wamekuwa wakihoji ikiwa nchi hiyo iko tayari kwa uchaguzi.Takriban watu milioni 6.8 walikuwa na uwezo wa kupiga kura katika vituo 21,000 kote nchini.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :