SCHWEINSTEIGER MCHEZAJI BORA UJERUMANI, KOCHA BORA NI JUPP HEYNCKES!
Posted in
No comments
Monday, July 29, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Katika Kura iliyoendeshwa na Jarida la
Soka maarufu huko Germany, Kicker, na Kura kupigwa na Wanahabari 527 wa
Michezo, Schweinsteiger alizoa Kura 92 akifuatiwa na Ribery Kura 87 na
Muller 85.
Katika Uchaguzi huo wa Mchezaji Bora, 10
Bora ilitawaliwa na Wachezaji wa Bayern Munich na Borussia Dortmund na
Mchezaji pekee wa Klabu nyingine alikuwa ni Stefan Kiessling.
Schweinsteiger, mwenye Miaka 28,
atakabidhiwa Tuzo yake kabla ya Mechi ya ufunguzi ya Msimu mpya wa
Bundesliga kati ya Bayern na Borussia Monchengladbach hapo Agosti 9.
Akiongelea kutunukiwa Tuzo hiyo,
Schweinsteiger alisema: “Taji hili ni kwa Timu. Imenishangaza kwani kuna
wakati vitu vibaya vilizungumzwa dhidi yangu!”
Nae Heynckes alitamka: “Hii ni kilele cha hadithi njema! Ndoto nyingi huwa kweli! ”
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :