LIVERPOOL YAPIGA CHINI OFA YA PAUNI 40 ZA ARSENAL KWA SUAREZ

Posted in
No comments
Wednesday, July 24, 2013 By danielmjema.blogspot.com

LIVERPOOL imeikataa Ofa nyingine ya Arsenal ya Pauni Milioni 40,000,001 kwa ajili ya kumnunua Straika kutoka Uruguay, Luis Suarez. 
 
Ofa hii, yenye idadi ya Fedha ya ajabu kidogo, ni ya makusudi ili ‘kuamsha’ Kipengele cha Mkataba wa Suarez ambacho kinaitaka Liverpool kutafakari Ofa yeyote ya kumnunua Suarez itakayotolewa ikiwa tu imevuka Pauni Milioni 40 na pia ni wajibu Mchezaji huyo kujulishwa kuhusu Ofa hiyo.

Lakini, Kisheria, Liverpool hawawajibiki kumuuza na hivyo ndivyo walivyofanya kwa kuikataa Ofa hii ya sasa ya Arsenal.
Arsenal, ambao Rekodi yao ya juu kabisa kumnunua Mchezaji ni Pauni Milioni 15 walizoilipa Zenit St Petersburg kwa ajili ya Andrey Arshavin Januari 2009, walitoa Ofa ya kwanza kwa Liverpool ya Pauni Milioni 30 na kukataliwa na Liverpool.

Wiki iliyopita Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, alisema thamani halisi ya Luis Suarez ni sawa na Edinson Cavani ambae hivi karibuni alijiunga na Paris St-Germain kwa Dau la Pauni Milioni 55.
Mbali ya Arsenal kumwandama Suarez, Real Madrid nayo inadaiwa kumtaka Straika huyo lakini bado haijatoa Ofa rasmi.

Kwa sasa, Suarez, ambae mwenyewe ameonyesha nia ya kuihama Liverpool lakini anapendelea aende nje ya England, yupo huko Australia pamoja na Liverpool ambao leo wanacheza Mechi ya Kirafiki na Klabu ya Melbourne Victory.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .