MATOKEO YA AWALI: KIONGOZI WA ZAMANI AONGOZA UCHAGUZI MKUU MALI
Posted in
No comments
Wednesday, July 31, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Waziri Mkuu wa zamani nchini
Mali Ibrahim Boubakar Keita anaongoza kwa kura za Urais, katika uchaguzi
unaonuia kurejesha utawala wa demokrasia nchini humo. Duru za serikali
zinasema aliyekua Waziri wa Fedha, Soumaila Cisse anafuata bw keita,
huku thuluthi moja ya kura ikiwa imehesabiwa.
Vuguguvu la Ukombozi wa jamii ya Tuareg ikisaidiana na wapiganaji wa kiisilamu walitwaa eneo nzima la Kaskazini, kabla ya muungano huo kusambaratika. Makundi hayo yalifanikiwa kunyakua Kaskazini mwa nchi baada ya jeshi kuipindua serikali ya kiraia ikilalamikia kutopata ufadhili kukabiliana na maasi Kaskazini mwa nchi.
Mapema mwezi huu, kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilitumwa Mali ili kusaidia katika shughuli za uchaguzi na kurejesha utawala wa kidemokrasia.Ufaransa umepongeza uchaguzi wa Mali, huku Muungano wa Ulaya ukisema shughuli hiyo ilifanyika bila visa vyovyote. Bw Keita maarufu kama "IBK" ana sifa ya kuwa na mabavu.
Mwanasiasa huyo aliendesha kampeini yake kwa ujumbe wa kurejesha hadhi kwa Mali akisema taifa liliisha hadhi yake kwa kuomba msaada wa Ufaransa ili kuinusuru dhidi ya kuporomoka.Viongozi wa kidini wengi wakiwa Waisilamu waliwaomba raia kumpigia kura, pia anaonekana kuungwa mkono na jeshi.
Bw. Cisse aliunda chama cha Union for the Republic and Democracy (URD) mwaka wa 2003 na ametaka jeshi kutojihusisha na siasa.Jumla ya wagombea 27 walichuana Urais, huku watu milioni 6.8 wakijiandikisha kupiga kura nchini Mali.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :