WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU
Posted in
Nishati
No comments
Thursday, January 8, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima akizungumza na wanakijiji wa Nyanguge wilayani Bariadi juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme iliyowekwa na REA. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. Profesa Sospeter Muhongo leo amezindua mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, mkoani Simiyu ambapo vijiji 170 vimeunganishwa na mradi huo. Ninawasilisha picha za matukio pamoja na captions kwa ajili ya kuchapishwa kwenye vyombo vyenu vya habari ili kuhabarisha umma. Aidha, captions zinapatikana mwishoni mwa email hii. |
Mwananchi kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye thamani ya shilingi bilioni 25.7. |
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu. |
Sehemu ya watoto kutoka katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili. |
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :