Showing posts with label Nishati. Show all posts
Showing posts with label Nishati. Show all posts

Gesi nyingine yagundulika Tanzania

Gesi nyingine yagundulika Tanzania

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Unaweza kuupata mwendelezo wote kwenye hii video…

NAIBU WAZIRI WA NISAHATI NA MADINI AKUTANA NA MAMENEJA WA TANESCO,MKOA LINDI, MTWARA, PWANI NA DAR ES SALAAM

NAIBU WAZIRI WA NISAHATI NA MADINI AKUTANA NA MAMENEJA WA TANESCO,MKOA LINDI, MTWARA, PWANI NA DAR ES SALAAM

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (katikati) akiwa katika kikao kilichojumuisha watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kulia kwa Waziri ni, Mhandisi Nishati Mwandamizi, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Salum Inegeja na kushoto ni Mhandisi Thomas Visi, Meneja wa kampuni ya Naomis Corporate Ltd inayotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini katika mkoa wa Mtwara.
Mhandisi Mkuu Usambazaji Umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Benedict Lyaruu (wa kwanza kulia), Kaimu Meneja wa TANESCO, mkoa wa Pwani, Eng. Rehema Mashinji (katikati) na Mhandisi Miradi ya Umeme katika mkoa wa Pwani, Leo Mwakatobe (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (haonekani pichani) wakati wa kikao chake na watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika miko ya Lindi na Mtwara.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mbele, katikati) akiwa katika kikao kilichojumuisha watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kulia kwa Waziri ni, Mhandisi Nishati Mwandamizi, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Salum Inegeja (kulia) na kushoto ni Mhandisi Thomas Visi, Meneja wa kampuni ya Naomis Corporate Ltd inayotekeleza miradi ya usambazaji umeme katika mkoa wa Mtwara.
Mhandisi Miradi ya Umeme katika mkoa wa Pwani, Leo Mwakatobe (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme katika mkoa wa Pwani mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (haonekani katika picha). Wa kwanza kulia mstari wa mbele, ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es salaam na Pwani inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara, Mhandisi Mahende Mugaya na wengine ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini.
Meneja wa TANESCO mkoa wa Lindi, Mhandisi John Bandiye akitoa taarifa ya miradi ya usambazaji umeme vijijini katika mkoa wa Lindi, mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (haonekani katika picha).Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Pwani.

WADAU WA NISHATI WAKUTANA KUJADILI MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA DUNIA NA ATHARI ZAKE KWA NCHI.

WADAU WA NISHATI WAKUTANA KUJADILI MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA DUNIA NA ATHARI ZAKE KWA NCHI.

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Bw. Allan William mtaalamu wa sekta za kibenki nchini, akizungumza katika mhadhara na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa juu ya Mwenendo wa bei za mafuta duniani  na athari zake kwa nchi yetu, mhadhara huo umefanyika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa JNICC uliopo jijini Dar es Salaam mapema leo Asubuhi.

Balozi Simba Yahaya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati (wa kwanza kulia), Balozi Mbelwa Kairuki (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Austrasia na Bw. Togolani Mavura kwa pamoja wakimsikiliza kwa makini Bw. Allan William.
Maafisa wa Wizara wakisikiliza kwa makini 
Balozi Simba Akichangia mada katika muadhara huo.
Bw. Adam Elinawinga kutoka kampuni ya PUMA naye akiendelea kuelezea mwendendo mzima wa bei za mafuta duniani na athari zake kwa nchi yetu. 

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima akizungumza na wanakijiji wa Nyanguge wilayani Bariadi juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme iliyowekwa na REA. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. Profesa Sospeter Muhongo leo amezindua mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, mkoani Simiyu ambapo vijiji 170 vimeunganishwa na mradi huo. Ninawasilisha picha za matukio pamoja na captions kwa ajili ya kuchapishwa kwenye vyombo vyenu vya habari ili kuhabarisha umma. Aidha, captions zinapatikana mwishoni mwa email hii.

Mwananchi kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye thamani ya shilingi bilioni 25.7.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Sehemu ya watoto kutoka katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI.

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza ziara katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho kushoto) ya kuitaka Tanesco kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme vijijini.

Sehemu ya umati wa wananchi wa kata ya Kalemala wilayani Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw. Steve Thomson (kushoto).
Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani).
Mkazi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega ambaye jina lake halikupatikana mara moja akitoa hoja yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele) mara Waziri alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi.

TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
Katika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari “Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya”. Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:

Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)

Taarifa za gazeti hilo zilieleza kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika uongozi wa Waziri Muhongo umekuwa ni wa kukatisha tamaa. 

Moja ya mifano iliyotolewa ni kuendelea kuwepo kwa wachimbaji madini wanaozidi kutorosha madini kwa nia ya kukwepa kodi. Hoja hii haina ukweli wowote kwani chini ya uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) utendaji wa Wizara umeimarika kwa kiasi kikubwa. Chini ya Uongozi wake kumekuwepo na uwajibikaji mkubwa kwa watumishi wa wizara ili kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi ipasavyo. 

Ni katika kipindi chake kumekuwepo na uanzishwaji wa madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vikubwa vya ndege vya JNIA, KIA na Mwanza chini ya Wakala wa Ukaguzi wa madini (TMAA) ili kudhiditi wachimbaji madini na watu wengine wenye nia ya kutorosha madini nje ya nchi bila kuzingatia sheria. Kutokana na hatua hiyo madini mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15 yameweza kukamatwa. 

Madini yaliyokatwa bila kuwa na vibali halali yametaifishwa na Serikali. Serikali ilianza kuuza baadhi ya madini yaliyokamatwa kwa njia ya mnada kwenye Maonyesho ya Vito yaliyofanyika Mjini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2014. 

Katika mnada huo jumla ya zaidi ya shilingi milioni 70 zilipatikana na kuingia Serikalini. Serikali itaendelea kupiga mnada madini mengine yaliyokamatwa kwa manufaa ya taifa. Wizara inaendelea kuimarisha udhibiti ili kuhakikisha kuwa mtu yeyote anayekusudia kutorosha madini anakamatwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na madini yake kutaifishwa na Serikali.

Katika kusimamia sheria na taratibu, chini ya Uongozi wa Prof.Muhongo, Wizara imedhibiti tabia ya kuchukua vitalu vya madini na kuhodhi ili wale tu wanaozingatia masharti ya leseni ndio waendelee kuvifanyia kazi vitalu. 

Hili limewaumiza waliokuwa na tabia hiyo ambao kimsingi walikuwa wanavunja sheria. Baadhi ya vitalu vilivyopokonywa vimekuwa vikigawiwa kwa wachimbaji wadogo.Hivyo, si kweli kwamba utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini chini ya Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ni wa kukatisha tamaa katika kudhibiti utoroshaji wa madini nje ya nchi na katika ukiukwaji wa masharti ya leseni mbalimbali za madini kama ilivyodaiwa.

Upitiaji Mikataba ya Madini

Taarifa za gazeti hilo la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 zilieleza kuwa chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) Serikali imeshindwa kupitia mikataba ya madini ili taifa linufaike zaidi. Taarifa hizo si za kweli zinalenga kupotosha umma.

Ukweli ni kuwa chini ya Uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb), Wizara imepitia mikataba ya madini kwa kufanya majadiliano na Kampuni za uchimbaji madini zenye mikataba ili kurekebisha vipengele vya mikataba ambavyo vinalenga kuleta manufaa zaidi kwa Taifa. 

Kazi hiyo imefanyika kwa Kampuni zote zenye mikataba na tarehe 9 Oktoba, 2014 Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) imetiliana saini mkataba wa kurekebisha vipengele katika mkataba uliosainiwa huko nyuma baada ya majadiliano kukamilika.

Aidha, majadiliano na Kampuni ya ACACIA (zamani Kampuni ya African Barrick Gold –ABG) yamekamilika na kilichobaki ni pande mbili (Serikali na Kampuni) kusaini marekebisho yaliyofanyika kwa ajili ya mikataba ya migodi yake ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.
  1. KUKATIKA KWA UMEME

Kukatika kwa umeme kunasababishwa na kuzeeka kwa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme. Ikumbukwe kuwa, kwa kipindi cha karibu miaka kumi TANESCO iliwekwa chini ya PSRC kwa nia ya kubinafsishwa mwaka 1997 – 2007. 


Katika kipindi hiki TANESCO haikuruhusiwa kuwekeza wala kufanya ukarabati wa miundombinu yake hivyo hali hiyo ilipelekea kuchakaa kwa miundombinu hiyo ikiwemo mfumo wa usafirishaji na usambazaji wa umeme. Hata hivyo baada ya Serikali kubadili mtazamo wake wa kulibinafsisha Shirika, TANESCO mipango kabambe ya kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo na kujenga mipya ili kuwa na mfumo wa usafirishaji na usambazaji umeme ulio wa uhakika. Kazi hiyo inaendelea katika sehemu mbalimbali nchini ikiwemo jiji la Dar es Salaam ambako kazi ya kukarabati na kupanua miundombinu ya usambazaji umeme inaendelea.

 Aidha, TANESCO ilishaelekezwa kutoa taarifa kwa umma kuhusu katizo lolote la umeme lililopangwa kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya umeme. TANESCO imekuwa ikifanya hivyo kwa kutumia vyombo vya habari vikiwemo televisheni, radio na magazeti na pia kwa kutumia magari ya TANESCO kufikisha taarifa kwa maeneo yanayoathirika. Kwa upande wa katizo la umeme usiotarajiwa, TANESCO inacho kikosi cha dharura ambacho watumishi wake wanafanya kazi masaa ishirini na nne kwa zamu ili kuhakikisha kuwa hitilafu ndogondogo zinatatuliwa mara moja zinapojitokeza. Jamii ya Watanzania wanalishuhudia hilo.


  1. DENI LA TANESCO LAPAA.

Mpaka kufikia mwanzoni mwa mwaka 2014, deni la TANESCO lilikuwa limefikia takribani Shilingi bilioni 695.30. TANESCO kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha kutokana na ukusunyaji wa maduhuli ndani ya kipindi cha miezi 11 imepunguza deni hilo mpaka kufika takribani Shilingi bilioni 355.11. Kukua kwa deni la TANESCO kulisababishwa na hali ya ukame uliolikumba taifa kuanzia miaka ya 2011 ambapo TANESCO ililazimika kununua umeme aghali kutoka kwa wazalishaji wa umeme binafsi ikiwemo mitambo ya kukodi ya dharura. Deni hilo lilikua kama ifuatavyo:

Mwaka Deni (Bilioni Sh.)
2011           538.47
2012            563.02
2013           695.30
2014 (9 Disemba) 355,11

TANESCO imeongeza ufanisi wake katika kukusanya maduhuri na kufikia kiwango cha asilimia 97 na fedha inayopatikana inatumika kupanua huduma ya umeme nchini, kuendesha Shirika na kulipa madeni inayodaiwa.

Ukweli ni kwamba deni la TANESCO limeshuka kwa kiasi kikubwa na kwa sasa TANESCO imeweka mkakati maalumu wa kuwalipa wadeni wake wakubwa kiasi cha Shilingi bilioni tatu kwa wiki kwa kila mdai, hivyo ni matarajio ya Shirika kumaliza deni hilo mwaka kesho (2015).

  1. NCHI ITASONGA MBELE

Wazo la kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lilibuniwa na watumishi na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2005/6 chini ya uongozi wa Nazir Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Taratibu za kuanzishwa kwa REA zilikamilika mwaka 2007 ambapo REA ilianza kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Sospeter Muhongo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ameisaidia REA kupata fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo amesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kwa kasi ya kupeleka huduma ya umeme vijijini.

Aidha, Ili kufikia lengo la kuwaunganishia umeme asilimia 30 ya watanzania ifikapo mwaka 2015, Chini ya uongozi wa Waziri Muhongo Serikali kupitia TANESCO, ilipunguza gharama za kuunganisha umeme wa njia moja (single phase) kwa wateja wadogo kwa wastani wa kati ya asilimia 30 na 77 kama ifuatavyo:

  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) kwenye umbali usiozidi mita 30 bila kuhitaji nguzo, katika maeneo ya vijijini watalipa Shilingi 177,000na wa mijini watalipa Shilingi 320,960 badala ya Shilingi 455,108 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.


  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) na kuwekewa nguzo moja, katika maeneo ya vijijini ni Shilingi 337,740 na wa mijini ni Shilingi 515,618badala ya Shilingi 1,351,884 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.


  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja na kuwekewa nguzo mbili katika maeneo ya vijijini ni Shilingi454,654 na wa mijini ni Shilingi 696,670 badala ya Shilingi 2,001,422 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.


Kwa ujumla katika kipindi hiki huduma ya umeme nchini imepanuka na kuwa bora zaidi kuliko siku za nyuma. Ni matarajio ya Serikali kuwa huduma hii itazidi kuwa bora zaidi katika siku chache zijazo kutokana na juhudi kubwa zinazoendelea katika sekta ndogo ya umeme.

  1. DALALI WA FEDHA ZA ESCROW

Waziri wa Nishati na Madini ndiye msimamizi mkuu wa masuala yanayohusu sekta za Nishati na Madini nchini. Mtambo wa IPTL ulijengwa kwa ajili ya kufua umeme unaotumiwa na jamii ya watanzania. Kuwepo kwa mgogoro kungeweza kuondoa azma ya uwepo wa mtambo huo ya kufua umeme ili kuliepusha Taifa kuingia katika mgawo wa umeme kutokana na upungufu wa upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo lilikuwa ni jukumu lake kuona kuwa mgogoro wa wawekezaji wa mitambo ya IPTL unakwisha ili mitambo iendelee kutoa huduma ya umeme kwa Taifa.

Jukumu la Waziri ni kusimamia Sera, Sheria na taratibu katika sekta anazozisimamia. Katika kufanya hivyo, Waziri hukutana na wadau na kujadili masuala kwa uwazi bila kificho kwa nia ya kujenga nchi na kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa ndiyo kipaumbele.

Kwa hiyo mikutano na Wadau ikiwa ni pamoja na wawekezaji hufanyika si kwa udalali. Suala la fedha za akaunti ya Escrow lilihusu uamuzi wa mahakama iliyojiridhisha kuwa mnunuzi wa hisa zote za VIP na MECHMAR ni halali na alitakiwa kukabidhiwa mali na madeni ya IPTL. Mali ni pamoja na kiasi cha fedha stahiki kwenye Akaunti ya Escrow ambazo hata hivyo ilidhihirika kuwa hazitoshi kukidhi deni halali.

Akaunti hiyo ilikuwa na Sh. 182 bilioni wakati malipo yaliyokubalika kwa pande zote (IPTL na TANESCO) kwa mujibu wa maamuzi ya ICSID I yalikuwa Sh. 306 bilioni. Kumwita Waziri wa Nishati na Madini kuwa ni dalali ni kupotosha ukweli.

WATANZANIA WASHAURIWA KUITUMIA NEEMA YA GESI KUPELEKA HIFADHI YA JAMII KWA KILA MTU

WATANZANIA WASHAURIWA KUITUMIA NEEMA YA GESI KUPELEKA HIFADHI YA JAMII KWA KILA MTU

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
DSC_0013
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,na Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh. Aggrey Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi karibuni katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC).(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Arusha.

MTAALAMU mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, ameishauri serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa wananchi wake.

Dhliwayo alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi wa jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii kwa wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka 2025 ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.

Dk. Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa na Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini Zimbabwe na Msumbiji. Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.

DSC_0005
Ofisa anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi. Usha Mishra akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na kutoa mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Alisema ipo nchi ambayo ilitumia utajiri wake wa almasi kutengeneza miundombinu ya barabara na si vibaya kwa Tanzania kutumia utajiri wake wa gesi kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.

Alisema kama taifa linaweza kuamua asilimia Fulani kutoka katika sekta ya gesi kuingia katika kuwezesha hifadhi ya jamii ambayo itahakikisha uwapo wa huduma sawa kwa wote. Alisema uchumi wa Tanzania kutoka mwaka 2000 hadi sasa umekuwa ukikua kwa kasi ingawa kasi hiyo haionekani kwa wananchi ambapo wengi wamejikuta wakiwa katika umaskini wa kukithiri.

Alisema kutokana na tatizo hilo la umaskini wa kukithiri kutoondoka kwa hali hiyo kunasababisha na sekta husika kutotoa ajira za kutosha ambazo zingewezesha watu kuneemeka na uchumi unaokua kwa kasi.

DSC_0079
Mtaalamu wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa mada chokonozi wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ambao umemalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Alisema aidha kaya nyingi zimekuwa na idadi kubwa ya watu ikiakisi umaskini unaoambatana na kaya zenye watu wengi na uzazi wa mapema unaowakuta wasichana. Alisema pamoja na mpango mzuri wa serikali kupitia TASAF kupunguza umaskini wa kukithiri ukishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu unawezesha mipango ya kupunguza umaskini inafanikiwa.

Alisema iwapo TASAF inashughulikia elimu na afya ni dhahiri itahitaji kuwapo kwa shule na walimu na katika afya hospitali na wauguzi na madaktari na dawa.” Ni lazima kuwepo na uratibu ili kufanikisha yote yaliyolengwa” alisema Dhliwayo.

Alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka mataifa ya Rwanda na Eritrea ambayo yamefanikiwa hifadhi ya jamii eneo la afya kufikia zaidi ya asilimia 90 huku wakitumia mifumo thabiti ya afya ya jamii kwa kaya.

DSC_0093
Kuki Tarimo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitoa mada chonokonozi wakati wa mkutano huo.

Aidha amesema kwamba mataifa hayo yamefanikiwa katika malengo ya millennia na kupunguza idadi ya vifo vya wanawake katika uzazi. Katika mkutano huo ambao uliitishwa na serikali ili kupata misingi ya utengenezaji wa sera na sheria ili kuwezesha watanzania wote kuwa na haki katika kei ya taifa kw akuwezeshwa kuondokana na umaskini wa kukithiri ulihudhuriwa na watalaamu 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Pia ulifunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi ambaye alisema Tanzania kwa sasa inapojianda kuwa na uchumi wa kipato cha kati ipo haja ya kuimarisha sekta za hifadhi ya jamii.

DSC_0101
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster akichangia hoja wakati wa mkutano huo uliomalizika hivi karibuni.
DSC_0109
Meneja Mwendeshaji wa Shirika la Under The Same Sun, Gamariel Mboya akiuliza swali kuhusiana na serikali imejipangaje katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi wanapataje mafuta ya kuzuia mionzi ya jua inayopelekea ugonjwa kansa ya ngozi.
DSC_0135
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe, akijibu swali kuhusiana na serikali imefanya nini kwa walemavu wa ngozi katika kuhakikisha mafuta kuzuia mionzi ya jua kwa watu hao yanapatikana kiurahisi ili kupunguza athari za kansa kwa walemavu hao. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
DSC_0159
Mwakilishi wa wazee waliostaafu akiuliza swali kwa Wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhusiana na uboreshwaji wa huduma za afya kwa wazee ambapo imekuwa changamoto kubwa kwao.
DSC_0025
Ujumbe wa Makatibu wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukishiriki wa mkutano huo.
DSC_0115
Mtaalamu wa mawasiliano wa Shirika la UNICEF Tanzania, Jacqueline Namfua akifurahi jambo wakati wa mkutano huo.
DSC_0029
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.
DSC_0107 DSC_0128 DSC_0067
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye mkutano.

SERA MADHUBUTI YA GESI KUINYAYUA TANZANIA

SERA MADHUBUTI YA GESI KUINYAYUA TANZANIA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mipawa to Ghana
Meneja wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa (kushoto) akielekea kukwea pipa kuelekea nchini Ghana kwenye ziara ya mafunzo ya wiki mbili.

Na Marco Mipawa, Accra- Ghana
Tanzania inaweza kuwa nchi ya kwanza katika maendeleo ya uchumi iwapo itaweka sera madhubuti za uzalishaji wa Gesi na kuwa na viongozi wenye dhamira dhabiti ya kuiendeleza nchi na kuboresha maisha ya watu.

Haya yamebainishwa na Meneja wa Redio Kahama FM Marco Mipawa leo wakati akiendelea na ziara ya mafunzo nchini Ghana ya kujionea jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi na jamii katika suala zima la maendeleo.

Mipawa ameyasema hayo baada ya kuona kuwa nchi ya Ghana inalo tatizo kubwa la upatikanaji wa nishati ya umeme hata kuliko Tanzania inavyoathirika na tatizo hilo lakini maisha ya watu ni mazuri na uchumi uko juu.

Amesema, katika jiji la Accra umeme hukatika takriban robo tatu ya siku na matumizi ya jenerata ni makubwa lakini thamani ya pesa yao iko kubwa ikilinganishwa na ya Tanzania ambapo kukatikakatika kwa umeme ni mara chache.

Mipawa amesema, dola moja ya marekani inathamanishwa na Sedisi tatu za Ghana ikiwa ni sawa na Shilingi 1770 za Tanzania hali inayoonyesha uchumi wa Tanzania uko chini ukilinganishwa na wa Ghana.

Baadhi ya wananchi wa Accra wamemwambia Mipawa kuwa, kinachoisaidia nchi ya Ghana ni Uzalishaji mali katika kilimo, madini na ufugaji; huku sera na sheria za nchi zikisimamiwa kwa umakini mkubwa kwa maslahi ya nchi.

Wamesema suala la kudhibiti rushwa na kusimamia utii wa sheria vikiambatana na uwazi na ukweli wa serikali na viongozi wa Ghana, ndiyo silaha mahususi zilizoifanya Ghana kuwa na uchumi imara na maisha mazuri ya watu.

Ziara ya mafunzo ya wiki mbili ya kujionea utendaji wa vyombo vya habari nchini Ghana, imehusisha watu tisa kutoka Tanzania wakiwemo waandishi wa habari na viongozi wa vyombo vya habari mbalimbali kwa udhamini wa Tanzania Media Fund (TMF).

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .