NAIBU WAZIRI WA NISAHATI NA MADINI AKUTANA NA MAMENEJA WA TANESCO,MKOA LINDI, MTWARA, PWANI NA DAR ES SALAAM
Posted in
Nishati
No comments
Wednesday, February 25, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
![]() |
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (katikati) akiwa katika kikao kilichojumuisha watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kulia kwa Waziri ni, Mhandisi Nishati Mwandamizi, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Salum Inegeja na kushoto ni Mhandisi Thomas Visi, Meneja wa kampuni ya Naomis Corporate Ltd inayotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini katika mkoa wa Mtwara. |
![]() |
Mhandisi Mkuu Usambazaji Umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Benedict Lyaruu (wa kwanza kulia), Kaimu Meneja wa TANESCO, mkoa wa Pwani, Eng. Rehema Mashinji (katikati) na Mhandisi Miradi ya Umeme katika mkoa wa Pwani, Leo Mwakatobe (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (haonekani pichani) wakati wa kikao chake na watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika miko ya Lindi na Mtwara. |
![]() |
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mbele, katikati) akiwa katika kikao kilichojumuisha watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kulia kwa Waziri ni, Mhandisi Nishati Mwandamizi, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Salum Inegeja (kulia) na kushoto ni Mhandisi Thomas Visi, Meneja wa kampuni ya Naomis Corporate Ltd inayotekeleza miradi ya usambazaji umeme katika mkoa wa Mtwara. |
![]() |
Mhandisi Miradi ya Umeme katika mkoa wa Pwani, Leo Mwakatobe (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme katika mkoa wa Pwani mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (haonekani katika picha). Wa kwanza kulia mstari wa mbele, ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es salaam na Pwani inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara, Mhandisi Mahende Mugaya na wengine ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini. |
![]() |
Meneja wa TANESCO mkoa wa Lindi, Mhandisi John Bandiye akitoa taarifa ya miradi ya usambazaji umeme vijijini katika mkoa wa Lindi, mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (haonekani katika picha).Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Pwani. |
Habari Zingine
- Gesi nyingine yagundulika Tanzania
- NAIBU WAZIRI WA NISAHATI NA MADINI AKUTANA NA MAMENEJA WA TANESCO,MKOA LINDI, MTWARA, PWANI NA DAR ES SALAAM
- WADAU WA NISHATI WAKUTANA KUJADILI MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA DUNIA NA ATHARI ZAKE KWA NCHI.
- WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU
- WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI.
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :