MFAHAMU MANDELA...NI MIAKA 95 NA TANO SASA!...HAPPY BIRTH DAY MADIBA!!

Posted in
No comments
Wednesday, July 17, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Rais wa Kwanza na Baba wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Madiba Mandela, kwa sasa yuko Hospitalini akipiganai Maisha Yake huko Pretoria Afrika Kusini. akiwa anatimiza Miaka 95 kesho Julai 18 mwaka huu, Mandela anabaki kuwa Mtu muhimu sana katika ukombozi wa Bara la Afrika kama sio nchi yake, Afrika Kusini.

Nelson Mandela ambaye watu wengi wanamchukulia kama kielelezo cha Uzalendo, anabaki kuwa mtu pekee ambaye Dunia nzima itaendelea kuenzi Uwepo wake hata kama atatuondoka leo au hata Kesho.

Swali la kujiuliza ni Je, Wangapi wanamfahamu Mandela? Wangapi wanafahamu kwa undani ni wapi alikotoka Shujaa huyu wa bara la Afrika? katika kuhakikisha hilo, TAIFA LETU.com imaendaa Makala Fupi ili kuwafahamisha Wapenzi wa Mzee huyu ni wapi alikjotoka na yey ni nani hasa.

Baba yake mzazi alifariki wakati Mandela akiwa na umri wa miaka tisa. Kutoka wakati huo alilelewa na Jonintaba hadi wakati alipoitoroka familia hiyo baada ya kutaka Mandela aoe katika ndoa ambayo tayari ilikuwa imeshapangwa.
 
Wakati Nelson Mandela ‘Mzee Madiba’ alipoliongoza taifa la Afrika ya Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na kuibuka kuwa miongoni mwa viongozi mashujaa duniani, tunapaswa kujuiliza ni watu gani katika familia yake ambao walikuwa naye bega kwa bega wakimuunga mkono muda wote.

Baba yake mzazi alifariki wakati Mandela akiwa na umri wa miaka tisa. Kutoka wakati huo alilelewa na Jonintaba hadi wakati alipoitoroka familia hiyo baada ya kutaka Mandela aoe katika ndoa ambayo tayari ilikuwa imeshapangwa.

Tangu wakati Mandela alipoanza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta usawa kwa wote, ilitegemewa kuwa mke wake ndiye angekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. Mandela aliwahi kuwa na wake watatu katika historia ya maisha yake, ambapo mke wa mwisho alimuoa siku alipokuwa akiadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwake.

Madiba anatajwa kuwa katika kipindi chote cha historia yake amekuwa akiwaunga mkono watoto na upatikanaji wa elimu. Mfuko wa Nelson Mandela wa kusaidia watoto ni sehemu tu ya ushahidi wa mafanikio ya Mandela kuwasaidia watoto.

Mandela ni baba wa watoto sita. Watoto wanne aliwazaa na mke wake wa kwanza, Evelyn Mase na watoto wawili aliwazaa na mke wake wa pili, Winnie Madikizela.

Historia watoto wa Mandela

Wapo kati yao ambao hawakuwahi kwenda kumwona baba yao wakati akiwa gerezani.Watoto wake wote wawili wa kike aliowazaa na mke wa kwanza walikuwa wakitumia jina la Makazawie. Mtoto wake wa kwanza alifariki akiwa na umri wa miezi tisa na mtoto wa pili aliyejulikana kwa jina la Madiba Thembikile (Thembi) alifariki katika ajali ya gari mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 25.

Mandela alikuwa gerezani na hakuruhusiwa kwenda kuhudhuria mazishi ya mwanae.Mtoto mwingine, Makgatho alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi mwaka 2005. Mandela amekuwa mstari wa mbele kupiga vita virus vya HIV na Ukimwi akitumia namba 46664 ambayo ni namba yake alipokuwa gerezani kupiga kampeni.

Mke wake wa Kwanza alikuwa ni Evelyne

Mandela na Evelyn walidumu katika ndoa yao kwa miaka 13 kabla haijavunjika mwaka 1957. Evelyn alikuwa muumini wa dhehebu la Mashahidi wa Yehova ambalo lilikuwa haliruhusu waumini wake kushiriki kwenye siasa, hivyo muda wote hakujihusisha na siasa. Alifariki mwaka 2004.

Baada ya Evelyne alimuoa Winnie

Mandela alimwoa Winnie Madikizera mwaka 1958, ingawa muda mwingi hawakuishi pamoja kwasababu Mandela alikuwa akitumikia kifungo huku Winnie akijijengea umaarufu katika majukwaa ya siasa.

Alitalikiana na Winnie kabla ya Kumuoa Graca Machel

Kutokana na misuguano iliyoibuka ndani ya umaarufu wa kisiasa ya Mandela na winnie walijikuta wakipeana talaka mwaka 1994. Mwaka 1998, Mandela alimwoa Graca Machel ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Rais wa Msumbiji, Samora Machel.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .