SIMON REGIS WA NEW HABARI (2006) APATA SHAVU LA KUWAKILISHA TAIFA KATIKA MASHINDANO YA UCHORAJI WA KATUNI NCHINI ANGOLA
Posted in
No comments
Thursday, July 18, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHORA
katuni wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, amepata mwaliko katika
ukanda wa Afrika Mashariki na kupewa nafasi ya kushiriki katika Tamasha
la 10 la International Cartoon Luanda litakalo
fanyika Agosti 15 hadi 23 nchini Angola.
Mchora
Katuni wa New Habari 2006 Ltd, Simon Regis kushoto, ambaye amepata
mwaliko wa nchini Angola, akikabidhiwa zawadi ya mkoba kutoka kwa
mwanafunzi wake wa uchoraji, Meddy Jumanne, leo jijini Dar es Salaam
kama ishara ya kutambua mchango wake kisanaa.
Regis ambaye jina lake lilitolewa kupitia kurasa ya Facebook
ya Tamasha hilo na kumzungumza kuwa ndio mchora katuni pekee kutoka ukanda huu
wa Afrika Mashariki atakaye shiriki Tamasha hilo kubwa Duniani.
Regis aliambia Mtanzania alshtushwa sana na habari hizo
pindi alipozipata kupitia kwa watu wanaofatilia mtandao huo kasha alipoingia
kutazama akakuta ni kweli.
“Kiukweli kwangu ni faraja kubwa sana kwani litakuwa ndio
tamasha langu kubwa kushiriki tangu nianze kuchora Katuni, hivyo naomba
watanzania waniunge mkono katika kufanikisha hili,” alisema Regis.
Alisema kuwa kwake ameona ni kitu cha ajabu sana kwani tangu
aanze uchoraji ameweza kufanya tamasha moja tu kubwa hapa nchini lakini hilo
ndio limeweza kumpa nafasi ya kuwakilisha nchi kimataifa.
Alisema Tamasha hilo amablo litajumuisha wachoraji
mbalimbali kutoka kila pembe ya Dunia ambao wanachora katuni za magazetini.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :