MASHAHIDI WAWILI WAJIONDOA KWENYE KESI YA UHURU KENYATTA THE HAGUE

Posted in
No comments
Thursday, July 18, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Fatou Bensouda
Kiongozi wa Mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC Fatou Bensouda, amesema kuwa mashahidi wawili wametupilia mbali ushahidi wao katika kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
 Bi Bensouda alisema mashahidi nambari 5 na 426 wamefutilia mbali ushahidi wao kwa sababu za waswasi kuhusu usalama wao.

Aliongeza kuwa upande wa mashtaka, ulikuwa umefanya mashauriano na shahidi nambari 426 kumtaka abadili msimamo wake, lakini mazungmzo hayakufua dafu.

"upande wa mashtaka umefanya mazungumzo na shahidi 426 kujua ikiwa hatua zozote zinaweza kuchukuliwa kuodnoa wasiwasi wake pamoja na kumwezesha kuhudhuria kesi. Mazungumzo hayo, hata hivyo hayakufua dafu baada ya kusisitiza kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi wake, '' aliongeza kusema Bi Bensouda.

Hata hivyo mwendesha mashtaka aliwaaambia majaji kuwa ushahidi wao sio muhimu tena kwa ushahidi wake dhidi ya mtuhumiwa.

Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake Samwel Ruto wanakabiliano na Shutuma ya kuhusika katika Machafuko ya Baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2007 ambayo yalishuhudia zaidi ya 1000 wakipoteza maisha huku wengine wakipoteza makazi.

Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta itaanza kusikilizwa Novemba 12.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .