MWENYEKITI CCM MKOANI K'NJARO AWATAKA WATANZANIA KUACHA KUTUMIA MUDA MWINGI KUJADILI RASIMU YA KATIBA
Posted in
No comments
Saturday, September 14, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na Fadhili Athumani, Moshi
MWENYEKITI wa CCM mkoani
Kilimanjaro, Iddi Juma, amewataka Watanzania kuacha kutumia tabia ya kutumia muda
mwingi kujadili Katiba na badala yake kujikita katika shughuli za kuimarisha
uchumi pamoja na kutatua kero za wananchi.
Kauli ya kiongozi huyo, imekuja
wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakizunguka
nchi nzima kuwahamasisha wananchi kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba mpya
hasa muundo wa serikali wanayoitaka.
Juma alisema kwa sasa kila mahali
utakuta watu wakitumia muda mwingi wa wamekusanyana makundi makundi wakibishana
kuhusu Rasimu ya Katiba hasa muundo wa serikali na kusahau kuwa kuna haja ya
kujishughulisha ili kuimarisha uchumi wao na uchumi wa nchi.
Mwenyekiti huyo alisema kujadili Rasimu ya Katiba bila kufanya kazi
za maendeleo ni upuuzi utekelezaji Katiiba kunahitaji Fedha na hilo
halitawezekana kama wananchi pamoja na Viongozi hawatazinduka na kuona haja ya
kutmia muda wao vizuri.
“Viongozi sasa hivi sio wa
Chadema, CCM, NCCR-Mageuzi, TLP, vingozi wa dini pamoja na Wananchi wanatumia
muda mwingi kujadili ya Rasimu ya Katiba, utakuta watu wakiwa katika makundi
wakibishana kuhusu Rasimu, Viongozi hasa hawa wenzetu wanazunguka kila mahali
kuhamasisha maoni ya wananchi lakini wanasahau kuwahamasisha kufanya kazi”,
alisema Juma
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM
Moshi Manispaa, Elizabeth Minde akizungumza baada ya chama hicho kutoa msaada
wa fedha na vifaa vya nyumbani kwa waathirika wa janga la Moto lililotokea
katika mtaa wa sabasaba kata ya Soweto, September 10 mwaka huu, alisema swala
la muhimu ni kufanya kazi kwani mwenye njaa kamwe haitambui hata “ingepakwa
rangi nyeupe”.
Minde ambaye ni Mwanasheria
kitaaluma alisema endapo uchumi wa nchi utayumba, katiba kama ilivyo sheria
inaweza ikaonekana haifai hata kama ingekuwa vipengele vizuri kiasi gani.
Katika Hatua nyingine Watendaji
wa ngazi za chini wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamedaiwa kuhujumu ziara za
vingozi wa juu wa CCM mkoani hapo pamoja na kukwamisha shughuli za chama katika
maeneo wanayosimamia.
Malalamiko hayo yalitolewa jana na
Wajumbe wa Mkutano wa Chama hicho katika ziara katika ziara ya Chama cha
Mapinduzi katika Manispaa ya Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Wakiongozwa na
Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa, Iddi Juma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
huku wakionesha kuchoshwa na manyanyaso wanayopata mikononi mwa watendaji hao baadhi
ya WanaCCM katika kata za Soweto, Shirimatunda Kilimanjaro na Karanga walidai
watendaji hao wamekuwa wakihujumu ziara za vingozi wa juu wa chama hicho.
Katika mkutano na Wananachama wa
Chama cha Mapinduzi katika Kata hizo, Baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo
waliwaanyoshea kidole watendaji wa ngazi za chini wakiwemo makatibu wa kata na
wenyeviti wao kuwa kikwazo kikubwa katika ziara za viongozi wakuu wa chama
hicho.
Malalamiko hayo yalikuja baada ya
kuwepo kwa hali isiyokuwa ya kawaia ya kuwepo kwa mahudhurio duni ya wanachama
pamoja na taarifa za ziara hiyo kutolewa wiki mbili kabla ambapo ilidaiwa kuwa
kikwazo ni baadhi watendaji hasa watendaji wa kata za Karanga na Shirimatunda
ambao wanadaiiwa kuendekeza rushwa katika utendaji wao.
Hali iyo ilijitokeza baada ya
mkutano wa Mwenyekiti huyo katika kata ya karanga iliyojumuisha kata zote tatu
za Karanga, Shirimatunda na Soweto kuhudhuriwa na wanachama wachache pamoja na
taarifa za ziara ya kiongozi huyo kutolewa wiki tatu kabla ambapo idadi iliyohudhuria
kilikuwa hakizidi wanachama mia.
Akizungumzia malalamiko hayo za
wananchama hao, Iddi Juma ambaye alionesha kukerwa na hali hiyo, alisema kwa
sasa CCM imejipanga kuhakikisha kila mtu anawajibika katkaeneo lake la kazi na
kuahidi kufikisha malalamiko hayo katika sehemu husika ili wote wanaotuhmiwa
wawajibishwe.
“Hali hii inasikitisha sana,
wananchi wanatutegemea kama viongozi wao, Sifa ya kiongozi ni kuongoza katika
harakati za kutatua kero za mwananchi sio kuzidisha kero hizo, tutahakikisha
swala hili linafika sehemu husika na tutafuatilia”, alisema Juma
Naye Katibu wa CCM manispaa ya
Moshi, Aluu Segamba alisema kuwa Chama hakitavumilia uona watu wachache
wanainajisi Serikali na kuongeza kuwa watahakisha wanapambana na wahujumu
uchumi.
“Watendaji wamekuwa
wakilalamikiwa sana, kwa mfano watendaji wetu ambao tunawategemea kama chama
tawala wameamua kutuoni jinsi gani wanavyoweza kuinajisi Serikali tena mbele ya
macho yetu, mwakani tunaanza harakati za uchaguzi tunahitaji watu makini na
hata hawa wanaofanya kazi kwa mazoea tutawatimua wote” alisema Segamba.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :