SHAMBULIAO LA AL SHABAAB KENYA...MILIO YA RISASI YASIKIKA NDANI YA WESTGATE NAIROBI, WATU 69 WAPOTEZA MAISHA
Posted in
No comments
Monday, September 23, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Huku hali ya mshikemshike
ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka,
ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na
mikahawa zaidi ya themanini.
Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia
ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Inaarifiwa wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi umesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.
Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.
Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa.
Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaa waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.
Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya kenya kupelekeka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :