CCM YAWAPONGEZA MALINZI NA TENGA

Posted in
No comments
Tuesday, October 29, 2013 By danielmjema.blogspot.com

DAR ES SALAAM, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais Mstaafu wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Leodegar Tenga kwa uongozi wa kupigiwa mfano uliowezesha kuleta mapinduzi katika mifumo wa mchezo wa soka nchini.

Pia imemtumia salam za pongezi za dhati Rais Mpya wa TFF, Jamal Malinzi, na Uongozi wake wote mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliopatikana katika uchaguzi uliofanyika juzi, Oktoba 27, 2013 jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam, leo, na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye inasema Chama hicho kinaimani kubwa na Malinzi wa wenzake katika kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na uongozi uliomaliza muda wake sanjari na kuibua mbinu mpya zitakazoboresha na kuleta mapinduzi makubwa ya soka nchini.

Katika taarifa hiyo, Nape ameuasa uongozi mpya kujiepusha na jitihada za kujiendeleza binafsi na badala yake uwekeze katika soka na kuepusha migogoro isiyo na tija katika mchezo huo ambao kwa sasa ndio unaopendwa na Watanzania wengi.

“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako (Malinzi) na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka" alisema  Nape.

Nape amesema Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa migogoro imekuwa kwa sehemu kubwa chanzo cha kukwamisha sana maendeleo ya soka hapa nchini na hivyo kuwanyima Watanzania raha ambayo huitarajia kutoka kwenye mchezo huo na hasa pale timu zao zinapopata ushindi.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .