DK. SHEIN AFUNGUA SEMINA YA MAFUNZO KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA CCM NGAZI ZA MIKOA NA WILAYA NCHINI

Posted in
No comments
Monday, October 21, 2013 By danielmjema.blogspot.com

 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua semina ya
mafunzo ya siku nne kwa Watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini, leo katika
jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, Oktoba 21, 2013. Wapili kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (zanzibar) Vuai Ali Vuai.

 Kinana akimkaribisha Dk. Shein kufungua semina hiyo ya siku nne
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na kumkaribisha Kinana
 Mwanzoni kabisa:Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika ukumbini kwa ajili ya kufungua semina ya mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya, leo kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa. Nyuma ya Dk. Shein ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi
 Dk. Shein akimsalimia Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Mwigulu Nchemba
 Kisha akamsalimia Katibu wa NEC, Irikadi na Uenezi, Nape Nnauye
 Halafu Dk. Shein akaondoka Uwanja wa Ndege kwenda White House kufungua semina hiyo,
 Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda akiteta jambo na mjumbe mwenzake kabla ya kuanza semina hiyo. Kushoto ni Katibu Msaidizi kutoka Idara ya Itikadi na Uenezi, makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda
HAPO SAWA! Naibu Katibu Mkuu wa CCM inaelekea ndivyo alivyokuwa akimsapoti, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk Asha-Rose Migiro wakati wakizungumza jambo kabla ya semina hiyo kufunguliwa rasmi na Dk. Shein Dk. Shein akiwasili ukumbini huku akisindikizwa na Kinana na Mwigulu Nchemba

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika ukumbini
kwa ajili ya kufungua semina ya mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na
wilaya, leo kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.
 Wajumbe wakishangilia Dk. Shein alipoingia ukumbini
Katibu wa CCM mkoani Kilimanjaro, Steven Kazidi (wa pili kulia) akishangilia pamoja na wanachama wengine waliokuwa ukumbini
Kushangilia kukanoga kwa sana ukumbini

Wadau ukumbini
 Sekretarieti ikiwa kazini ukumbini
 Wakibadilishan mawazo
Wakibadilishana mawazo
Mzee Monga akiwa imara katika kuhakikisha semina inakwenda vizuri
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akitambulishwa ukumbini
NAWATAKIENI SEMINA NA MAFUNZO MEMA: Dk. Shein akiwaaga washiriki wa semina hiyo wakati akiondoka ukumbini baada ya kuifungua.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .